• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

“TUNAJIVUNIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NDANI YA MWAKA MMOJA” DED - NYANG’HWALE

Posted on: August 22nd, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imepongezwa kwa hatua kubwa ya maendeleo ya sekta mbalimbali kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hayo yamesemwa leo Agosti 22, 2024 kwenye Mkutano wa mwaka wa Baraza la Madiwani uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizofanyika kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Ndg. Husna Toni, amesema Halmashauri ilikasimia kukusanya  Tsh. Bilioni 3.2 za mapato ya ndani na imefanikiwa kukusanya Tsh. Bilioni 3.6 sawa na asilimia 112.5 ya malengo.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri imepokea Tsh. Bilioni 7.03 kutoka vyanzo mbalimbali zilizowezesha ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kutolea huduma ikiwemo Afya, Elimu, Utawala na Kilimo.

“Halmashauri ilipokea Tsh. Bilioni 2.1 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la utawala la Halmashauri, Ununuzi wa vifaa tiba katika hospitali ya Wilaya, vituo vya Afya na Zahanati” Amesema Ndg. Husna Toni

Fedha hizo pia zimetumika kukarabati Shule kongwe za Msingi za Mimbili na Nyang’hwale, kuchochea Mfuko wa jimbo, ukamilishaji wa Zahanati mbili katika Vijiji vya Kaboha na Isonda, ukamilishaji wa maabara Shule ya Sekondari Kaboha na Ujenzi wa bweni kwenye Shule ya Msingi Bupamba yenye watoto wenye mahitaji maalum.

Aidha, Kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Halmashauri ilipokea Tsh. Bilioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba tano za Watumishi katika Shule ya Msingi Ipalang’ombe, Ngelela, Nyamikonze, Shule ya Sekondari Nyabulanda, Kituo cha Afya Kafita, ujenzi wa jengo la OPD Kituo cha Afya Nyang’hwale na jengo la Wazazi  Zahanati ya Mwamakiliga.

Vilevile kupitia program ya BOOST, Halmashuri imepokea Tsh. Milioni 293.8 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika Shule za Msingi Madulu, Kharumwa na Nyakaswi.

Halmashauri kupitia program ya SEQUIP imepokea Tsh. Bilioni 1.5 kwa ajilii ya ujenzi wa Shule mpya Kata ya Kharumwa, Ujenzi wa mabweni 6 na matundu ya vyoo 28 kwenye Shule za Sekondari Busolwa, Bukwimba, Kanegele na ujenzi wa nyumba ya Mtumishi Shule ya Sekondari Kanegele.

Mkurugenzi Mtendaji amemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayoboresha mazingira ya kutolea huduma kwa Wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu na Afya.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved