• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

TAARIFA YA UGAWAJI WA VIFAA NA MASHINE

Posted on: August 25th, 2022

NDUGU MGENI RASMI (Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Rajabu Mmunda)

Shirika la SEDIT ni shirika lisilo la kiserikali lililosajiliwa mwaka 2005 linalojishughulisha na Ukuzaji wa kipato cha kaya,kuchochea ukuaji wa kiuchumikupitia kilimo biashara,uchocheaji wa huduma za afya utunzaji wa mazingira na usawa wa kijinsia, na utunzaji wa maliasili na Kuzijengea uwezo  endelevu taasisi juu ya mfumo wa kuweka na kukopa. 

Shirika la SEDIT kwa kushirikiana na shirika la Plan International, na shirika la  Kivulini kwa pamoja yanatekeleza Mradi wa Kutokomeza Ajira Hatarishi na Ukatili kwa Watoto awamu ya 3 (Mwaka 2020-2023) unaotekelezwa kwenye wilaya za Geita ,Nyang’hwale na Chato,Zenye  jumla ya kata 15  ambapo kati ya hizo, wilaya ya NYANGHWALE  ina inatekeleza kwenye kata 4 ambazo ni Shabaka,Busolwa,Nyijundu   na Nyamtukuza .Kata hizo zina  jumla ya Vijiji 14 ambapo mpaka kufikia mwezi Agosti 2022 mradi umefanikiwa kuunda jumla ya Vikundi vya hisa 54 ( kati ya vikundi 198 vya mradi kutoka kwenye Wilaya zote 3) vyenye jumla ya wanachama 1,138 (343 ME  na 795 KE ) ( kati ya wanachama  wote wa vikundi 4705 tulivyonavyo). Vikundi vyote 58 vimeweza kuwa na mtaji wa kiasi cha shilling 141,183,500/=( Kati ya milioni 600,000,000 walizonazo kwa vikundi vyote vya mradi ) ambazo wamezichanga wao wenyewe bila kupewa na mtu au taasisi yeyote ile.Sambamba na hili vikundi 27 vimesajiliwa kwa mujibu wa shereia ya huduma ndogo za fedha ya Mwaka 2018 na vikundi 27 vilivyobakia , taratibu zingine za usajili zinaendelea.

NDUGU MGENI RASMI

Kupitia vikundi hivi vya Hisa mradi umeweza kuwapatia mafunzo ya ujasiliamali kupitia kwa wawezeshaji         Jamii na kuwawezesha wanachama kuanzisha biashara na miradi ya mmoja mmoja na pia vimeanzisha miradi mbalimbali ya vikundi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mazao,ulimaji bustani,ufyatuaji wa tofali,useremala,ufugaji wa kuku ,ushonaji wa nguo n.k. Aidha ifahamike kuwa  vikundi 4 vya Vijana chini ya Miaka 25 vilipatiwa mafunzo stadi kwa kushirikiana na Shirirka la SIDO na Kuwawezesha Vijana 53( ushonaji 32,seremala 5,Ufugaji kuku 16) wa Wilaya ya NYANGHWALE  kupata Mafunzo yatakayowawezesha vijana kujiajiri ikiwa ni pamoja na Mafunzo ya Ufugaji wa Kuku na Ushonaji  na useremala. Vijana wote wameshahitimu mafunzo hayo na baaadhi yao utawagawia vitendea kazi hii leo.

NDUGU MGENI RASMI

Kutokana na jitihada zilizoonyeshwa na vikundi 12 (kati ya vikundi 58) vilivyoorodheshwa hapa chini katika ubunifu na Usimamizi wa  miradi mbalimbali ya vikundi kulingana na maeneo yao. Sisi kama Mradi na wadau wa Maendeleo tumeona ni vema kuwaunga mkono kwa kuwapatia vifaa mbalimbali ambavyo ni :-

  • Overlock Machine 1
  • Cherehani 8
  • Mashine ya Umwagiliaji 1
  • Mipira ya Umwagiliaji 1
  • Mashine za Kutotoleshea Vifaranga(Uwezo wa kutotolesha  mayai 264)  1
  • Mizinga ya nyuki 6.
  • Vifaa vya lishia na kunyweshea kuku

Vifaa/Mashine hizi zote kwa pamoja vina thamani ya shilingi 7,022,500/=, kati ya hizo kiasi cha shilingi 6,566,500/= zimetolewa na mradi  sawa na 94% na kiasi cha shilingi 456000/= zimechangwa na vikundi 1 katika ununuzi wa vifaa hivyo sawa na 6%. Ni matarajio ya Mradi kuwa vikundi vitavyokabidhiwa mashine hizi kwa siku ya  leo na  kesho,vitaenda kuvitumia vifaa hivi kwa malengo yaliyokusudiwa na kuongeza uzalishaji na kujiongezea kipato. Aidha vifaa hivi vitakwenda kuzalisha fursa za  Ajira kwa wanachama wanufaika wa Mradi na kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza wimbi la Vijana wasio na Ajira katika wilaya yetu ya Nyanghwale .

Tunatoa wito kwa vikundi vyote vitavyokabidhiwa vifaa hivi,viende vikawaunganishe na kuimarisha Maendeleo ya vikundi hasa Katika kipindi hiki kinachoelekea mwisho wa Mradi mwezi februari 2023. 

 

NDUGU MGENI RASMI

Tungependa utambue uwepo wa Mashirika wenza ambao ni Shirika la Plan Internatriona na Shirirka la Kivulini ambao kwapamoja na sisi tunatekeleza mradi mmoja wa Kutokomeza Ajira Hatarishi na Ukatili kwa watoto awamu ya 3.Baadi ya timu ya mradi  wameshindwa kuhudhuria kutokana na majukumu mbalimbalia ya kusukuma Maendeleo. Tunayo furaha sasa kukukabidhi vifaa na Mashine hizi vipya kabisa ili nawe uwakabidhi wawakilishi wa vikundi walioweza kufika leo .

Changamoto.

1. Kuna idadi kubwa ya vijana wanaohitaji vitendeakazi kama vile cherehani na vifaa vya kutotolesha vifaranga.Mf. kutokama na bajeti ya mradi tuliyokuwa nayo tumeweza kuwapatia vyerehani 9 tu kati ya vijana 59.Ombi letu tunaomba maafisa Maendeleo ili kuwafikia na kuona namna bora ya kuwasaidia kupata mkopo wa vitendea kazi na kuwezesha waweze kujiajiri.

2. Ufinyu wa bajeti katika kuyafikia maeneo yote ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyanghwale .

Vikundi vingi kuwa na miradi mizuri ya pamoja , lakini kutokana na ufinyu wa bajeti hatukuweza kutoa vifaa kwenye vikundi hivyo.Ombi letu Timu ya Maafisa Maendeleo kuendelea kuvitembelea na kuona namna bora ya kuwasaidia mikopo ya vitendea Kazi.

ORODHA YA VIKUNDI VITAVYOKABIDHIWA VIFAA.

NA
KIKUNDI
KIJIJI
KATA
VIFAA
IDADI
1
TUKWAMUANE -NYIJINDU NYANGHWALE
IYOGELO
NYIJUNDU
SETI YA VIFAA VYA KULISHIA KUKU
SETI 1
2
WACHAPA KAZI  SHABAKA
SHABAKA
SHABAKA
MASHINE YA KUTOTORESHEA VIFARANGA
 1
3
TUKWAMUANE SHABAKA
NYAMGOGWA
SHABAKA
VYEREHANI
2
4
UPENDO NYAMTUKUZA
NYAMTUKUZA
NYAMTUKUZA
VYEREHANI
2
5
UPENDO SHABAKA
IHUSHI
SHABAKA
WATER PUMP
1

UPENDO SHABAKA
IHUSHI
SHABAKA
MPIRA WA MAJI
1
6
UPENDO  NHWIGA NYAMTUKUZA  
NHWIGA
NYAMTUKUZA
MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI
6
7
UPENDO NYIJUNDU
IYOGELO
NYIJUNDU
CHEREHANI
2
8
KAZI NA MALENGO NYAMTUKUZA
NYAMTUKUZA
NYAMTUKUZA
CHEREHANI
2

Mwisho

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki NYANGHWALE .

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved