• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

RAS atoa Maagizo mazito Nyang'hwale

Posted on: April 12th, 2019

Katibu Tawala wa Mkoa wa Nyang’hwale Ndugu Denis Bandisa  amewataka Watumishi wa Halmashauri hiyo kujibu hoja themanini na tano zilizo kwenye makundi manne zilizopelekea  Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale kupata Hati Chafu kwa mwaka wa Fedha 2017/18 ripoti iliyosomwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Akiongea na Watumishi kwenye Ukumbi wa Halmashauri amesema, Watumishi wote wanapaswa kufanya hivyo mapema iwezekanavyo ili kufanya hoja hizo zifutwe na kuondoka kwenye Hoja hizo ili Halmashauri ipate Hati safi kwenye Hesabu zijazo.  

Aidha, Bandisa ameagiza kuchukuliwa hatua kwa wote waliosababisha Hoja hizo kama miongozo inavyohitaji ili kutoa fundisho kwa Watumishi wengine kuona umuhimu wa Kujibu oja kila wanapohitajika.

Kutokana na Udhaifu wa Menejimenti ya Halmashaurir kwenye kujibu hoja hizo, ameagiza kusitisha kwa taratibu zote zinazoendelea za kuwathibitisha Makaimu wote kwenye Idara na Vitengo wanavyovihudumia hadi Halmashauri itapopata Hati safi mwakani.

Bandisa amesisitiza Idara ya Fedha na Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani kuhakikisha wanaitoa Halmashauri ilipo na kusonga mbele kwa kushirikiana na sio kutupiana lawama. “shida zote, raha zote ziwe za wakuu wa Idara”… alisema.

Katika kufanikisha hayo, Mtaalamu wa Masuala ya kifedha kutoka Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa Ndugu Mabula amewataka Idara ya Fedha kuandaa Orodha ya Majedwali yaliyo na hoja zote 85, kuchambua Hoja na kuona ambazo hazijajibiwa kama zinahitaji majibu kwa msaada wa vielelezo kutoka Taasisi zingine, uimarishwaji wa Mifumo ya Fedha ni muhimu hasa Wadaiwa wa Fedha za Mapato na Vitabu vipatikane.

Bwana Mabula amesema majibu yasiyo ya kweli na yasiyo na uhakika hayatatutoa kwenye hoja hizo hivyo inatupasa kuwa weledi na waadilifu kweli kuhakikisha tunafanikisha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Hamim Gwiyama alisema Hati chafu tuliyopata ni matokeo ya Kukiuka taratibu za Kifedha, na kukosekana kwa umakini katika kazini akakgiza kuanzia kesho Watumishi wenye hoja waanze kujibu hoja hizo mara moja.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved