• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Plan Internatinal yainoa Kamati ya Kutokomeza Ukatili wa kijinsia Nyang’hwale

Posted on: February 28th, 2019

Shirika lisilo la Kiserikali la Plan International leo Alhamisi limeanza kutoa Mafunzo ya siku tatu yanayolenga kuwajengea uwezo wa Kutokomeza ukatili dhidi ya  Wanawake na Watoto kwa Kamati ya Wilaya hiyo yenye jukumu la Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto.

Akifungua Mafunzo hayo Mwenyekiti wa Kamati ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Mariam Chaurembo amewataka Wajumbe kusikiliza kwa makini Mafunzo hayo ili baada ya siku tatu hizo kila Mjumbe awe Mjumbe kwenye eneo lake kuhakikisha Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake Wilayani hapa unakomeshwa.

Bi Chaurembo  amewashukuru sana Shirika hilo kwa kuleta Mafunzo hayo Wilayani humo na amekiri tatizo la Ukatili wa Watoto na Wanawake lipo ambapo alitolea mfano Mwanafunzi wa Kidato cha pili shule ya sekondari Msalala aliyenyanyapaliwa baada ya kufariki wazazi wake kwa kuambiwa naye atakufa hivyo aliyeacha shule na kwenda kujiuza Maeneo ya Mgodini Kakola Wilayani Kahama ambaye alimbaini mwenyewe na akamrudisha shule.

Aidha, Mwenyekiti huyo alitaka kamati hiyo kuhakikisha inaleta matokeo chanya kwenye Jamii kwa kuhakikisha inawasaidia wananchi kujua ni matendo gani yana athari kwa makuzi, elimu, Uchumi na ustawi kwa ujumla kwa mtoto wa kike na mwanamke endapo atafanyiwa maana lipo tatizo la Jamii kufanya mambo pasipo kujua kuwa wanamnyima haki mtoto au mwanamke kutokana na matendo mengine kuwa ni ya kawaida kwenye Jamii husika.

Wakati akitoa mada ya Mpango kazi wa Kitaifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa mwaka 2016 hadi 2022,Mwezeshaji Ndugu Onesmo Itozya aliyataja maeneo nane ya Msingi ya kuzingatia ili kuhakikisha Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto unatokomezwa kuwa ni pamoja na dhana nzima ya jinsia, uwezeshaji Wanawake kiuchumi na kuzifahamu mila na desturi za Jamii inayotuzunguka.

Vilevile, alitaja kuwa lazima tufahamu maeneo salama ya Mazingira ya umma, malezi, msaada na Uhusiano. Huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili pia  alielezea kuwa ni muhimu kufahamu pamoja na Ulinzi na stadi za Maisha kwa Watoto Mashuleni.

Ndugu Itozya alimalizia maeneo hayo muhimu kwa kusema kuwa ni lazima mwanakamati ya wilaya afahamu taratibu za kuchukua endapo kuna muathirika wa ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto lakini pia kufanya tathimini na Ufuatiliaji ili kuweza kumsaidia muhanga watatizo.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved