• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Nyamikonze kupata Kituo cha Afya Julai

Posted on: April 27th, 2018

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nyang’hwale Ndugu Carlos Gwamagobe amewataka wananchi wa Kijiji cha Nyamikomze kumuunga Mkono Mhe. Mbunge kwenye Ujenzi wa Kituo cha Afya Nyamikonze ili Mwezi Julai kianze kutoa huduma kwa wananchi kwani hadi sasa imebaki miundombinu ya Choo, Kichomea Taka na Nyumba ya Watumishi ili kituo cha Afya Nyamikonze kianze kutoa Huduma. “Serikali imeamua Mwezi wa saba kuanza kutoa huduma za afya hapa” alieleza Mkurugenzi.

Ameeleza hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Muungano yaliyoambatana na Mkutano uliofanyika ndani ya Majengo ya Kituo hicho ambapo Menejimenti ya Halmashauri ilipowatembelea na kuzungumza na viongozi na wadau wa maendeleo kwenye kata hiyo.

Ndugu Gwamagobe amesisitiza umuhimu wa kituo hicho kwani wakazi wa maeneo hayo watapata huduma karibu tofauti na ilivyo hivi sasa.

Amewataka viongozi wote kwenye kata hiyo kuunganisha wananchi kwenye suala hilo ili wahamasike na kuweza kujitolewa kwa moyo na kuhakikisha wanapata ari ya kupata huduma ya afya kwa karibu.

Wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji, Mhe. Diwani wa kata ya Mwingiro ndugu Shilole alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kuwajali kwani pamoja na kwenda kuhamasisha numaliziaji wa Ujenzi huo pia amewaahidi kuwapatia gari la kubebea Wagonjwa mara tu kituo cha Afya kitapoanza kazi.

Aidha Mhe. Diwani alimuahidi Mkurugenzi kuwaunganisha wananchi na Viongozi wa kata hiyo kuhakikisha wanajitoa kwenye mapambano hayo.

Kata ya Mwingiro ina vijiji vine vya Mwingiro, Iyenze, Mwasabuka na Nyamikonze ambapo wananchi wa kata hiyo wanahudumiwa kwenye Zahanati ya Nyashilanga iliyo mbali na makazi yao.

Kata ya Mwingiro ipo kaskazini mwa Wilaya ya Nyanghwale na inapatikana KM 35 kutoka Makao makuu ya Wilaya ambapo wananchi wake wanajihusisha na shughuli za Kilimo, Ufugaji na Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu.

Mkutano huo uliambatana na Harambee ya Ujenzi ambapo jumla ya Fedha taslimu zaidi ya laki mbili zilitolewa na mifuko ya Saruji 118, Mbao 10 na Misumari kg 32 iliahidiwa kutolewa ndani ya wiki moja.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved