• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

HALMASHAURI YASAINI MKATABA NA KAMPUNI ZA URASIMISHAJI WA MAKAZI HOLELA

Posted on: September 18th, 2025

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale leo Septemba 18, 2025 imesaini Mkataba na Kampuni 12 za Urasimishaji wa Makazi holela katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.

Kaimu Mkurugenzi Ndg. Ezekiel Ntiriyo amezitaka Kampuni zilizosaini Mkataba huo kuzingatia masharti na makubaliano yaliyowekwa kwenye mkataba ili kufanya kazi kwa weledi.

Mkuu wa Idara ya Ardhi (W) Ndg, Mathias Bujiku amesema maeneo ambayo yatafikiwa na zoezi hilo ni pamoja na Kata ya Busolwa Kijiji cha Busolwa na Ifugandi, Kata ya Nyijundu Kijiji cha Nyijundu, Kata ya Kakora Kijiji cha Kakora na Kitongo.

Maeneo mengine ni Kata ya Nyang'hwale Kijiji cha Nyang'hwale, Kata ya Bukwimba Kijiji cha Bukwimba, Kata Izunya Kijiji cha Sweya na Kata ya Kharumwa Kijiji cha Kharumwa na Busengwa.

Mkurugenzi wa kampuni ya urasimishaji ya Wide Chance Ltd, Ndg, Siyaone Likombe amesema zoezi hilo litawasaidia Wananchi kutatua migogoro ya ardhi baina yao na kuongeza thamani ya ardhi wanayoimiliki.

"Zoezi hili linaenda kuwaongezea Wananchi usalama wa umiliki wa ardhi yao kwa sababu mwisho wa zoezi hili Wananchi watakabidhiwa nyaraka za umiliki wa ardhi ambazo ni hati miliki za kimila" Amefafanua

Rai imetolewa kwa Wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa makapuni hayo pindi yatakapofika kwenye maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi hili.

Kaimu Mkurugenzi Ndg. Ezekiel Ntiriyo akiwa kwenye kikao cha kusaini Mkataba na Kampuni za Urasimishaji wa Makazi.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 02, 2025
  • TANGAZO LA KUHAMA KWA STENDI YA MABASI YA ABIRIA KWENDA STENDI MPYA YA IKANGALA KUANZIA TAREHE 30/08/2025 August 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU August 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA MKATABA July 30, 2025
  • View All

Latest News

  • SHULE ZA SEKONDARI ZAKABIDHIWA MITUNGI YA GESI KUDHIBITI MAJANGA YA MOTO

    September 19, 2025
  • HALMASHAURI YASAINI MKATABA NA KAMPUNI ZA URASIMISHAJI WA MAKAZI HOLELA

    September 18, 2025
  • MAAFISA KILIMO NA MIFUGO WATAKIWA KUONGEZA UBUNIFU ILI KUWASAIDIA WAKULIMA KUZALISHA KWA TIJA

    September 18, 2025
  • WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA UANDAAJI WA MASHAMBA YA SHULE KUELEKEA MSIMU WA KILIMO

    September 16, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved