• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WAFANYAKAZI WA BANK YA CRDB NYANG'HWALE WAPEWA ELIMU YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Posted on: November 12th, 2025

Kuelekea Kilele Cha Maadhimisho ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza, Novemba 15, 2025. Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe, imetoa Elimu ya Magonjwa yasiyoambukiza kwenye Taasisi za Umma, binafsi na Wananchi.

Elimu hiyo imetolewa leo Novemba 12, 2025 kwa Watumishi wa Benki ya CRDB Nyang'hwale, Shule ya msingi Samia, Shule ya Mchepuo wa Kingereza Kharumwa na Shule ya Sekondari Nyijundu.

Elimu hiyo imetolewa na wataalamu Kutoka Hospitali ya Wilaya ya Nyang'hwale wakiongozwa na Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza Dkt, Zakia Mbulla.

Akizungumza wakati wa utoaji Elimu ya Magonjwa hayo Dkt, Zakia Mbulla amesema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa Elimu na Huduma za uchunguzi wa Magonjwa yasiyoambukiza kwa Watumishi na Wananchi kwa ujumla ili kubaini mapema Magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na uzito uliopitiliza.

Dkt, Zakia Mbulla amesema katika uchunguzi wa awali imebainika kuwa idadi kubwa ya watu wamekutwa na kiwango kikubwa cha Sukari sambamba na Shinikizo la damu, ambapo magonjwa haya yanasababishwa na mtindo wa maisha.

Kwa upande wake Afisa Lishe (W) Ndg, Somoe Bakari amesema tabia ya kula vyakula vilivyosindikwa viwandani husababisha ugonjwa wa Kisukari kwa sababu usindikaji wake unahusisha matumizi makubwa ya sukari.

Sambamba na hayo, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma, Ndg. Neema Mhoja amewashauri Watumishi kuwa na desturi ya kufanya mazoezi ambayo yanachangia kuondoa kiwango cha mafuta yaliyoganda mwilini na kuuweka mwili mbali na Magonjwa yasiyoambukiza.

Kilele Cha Maadhimisho hayo kitafanyika katika Uwanja wa Sabasaba Kharumwa kwa kufanya mazoezi ya viungo pamoja na Huduma za uchunguzi wa magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la damu, Saratani ya shingo ya kizazi, huduma ya kinywa na meno pamoja na Hali ya lishe.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 02, 2025
  • TANGAZO LA KUHAMA KWA STENDI YA MABASI YA ABIRIA KWENDA STENDI MPYA YA IKANGALA KUANZIA TAREHE 30/08/2025 August 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU August 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA MKATABA July 30, 2025
  • View All

Latest News

  • WAFANYAKAZI WA BANK YA CRDB NYANG'HWALE WAPEWA ELIMU YA KUJIKINGA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

    November 12, 2025
  • WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KWENDA KUSIMAMIA MIRADI KWA UFANISI

    November 07, 2025
  • MAFUNZO YATOLEWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO NA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA

    October 26, 2025
  • MILIONI 206 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 31 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU AWAMU YA KWANZA YA MWAKA 2025/2026

    October 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved