• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Nyang’hwale Kinara wa Huduma Bora za Afya Mkoani Geita

Posted on: July 26th, 2018

Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Faustine Ndugulile, amekabidhi Ngao kwa Mkurugenzi wa Halmashuri ya Nyang’hwale ambaye ameshinda Tathmini ya Matokeo Makubwa sasa (BRN) katika idara ya Afya kwa mwaka 2017/18 kupitia kigezo cha Upimaji wa Kiwango cha Utoaji Huduma katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa matokeo ya Upimaji wa Nyota za Ufanisi wa utoaji Huduma bora.

Akikabidhi Ngao hiyo leo asubuhi ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Naibu waziri amesema Wilaya ya Nyang’hwale imevuka lengo la Wizara kwa kupata alama zaidi ya asilimia 80 zilizowekwa na Wizara, ambapo wilaya hii imepata asilimia zaidi ya 93 na kwa kila kituo cha kutolea huduma za Afya tumepata alama ya  nyota tatu zinazokusudiwa na wizara.

Alipopokea taarifa ya Afya kutoka kwa kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta Joseph Odero na kuona kuwa kuna vifo 1470 vitokanavyo na Uzazi,Mhe Ndugulile alisisitiza wataalamu wa afya mkoani Geita kuhakikisha wanazuia vifo vitokanavyo na Uzazi kwani sababu ya vifo hivyo vingi zinazuilika ambapo alieleza kuwa ni mara chache kutokea vifo hivyo. Aidha, alifafanua sababu zake kuu tatu kuwa aidha mama amechelewa kuchukua maamuzi ya kwenda kwenye zahanati, pili mama amechelewa kufikishwa kwenye kituo cha kutolea huduma au mama amefika kwenye kituo cha kutolea huduma na kucheleweshwa kupata huduma sahihi.

Ameagiza kuwa, vituo vianze kutekeleza muongozo wa Wizara uliotolewa hivi karibuni ambao unawataka watoa huduma za Afya wote kuhakikisha kuwa kila mgonjwa/mteja afikapo kwenye kituo cha kuitolea huduma lazima iandikwe tarehe ya kumpokea na muda wake, kuanzia mapokezi, kwa tatibu au daktari, kwa Mtaalamu wa maabara na sehemu anapopatiwa dawa kwani hii itatumika katika ufuatiliaji na uhakiki wautoaji wa huduma bora nchi nzima.

Pia alizungumzia ugonjwa wa ukoma ambapo alisema Ugonjwa huu ni lazima kuutokomeza Katika Mkoa wa Geita kwa kuibua wagonjwa wa Ukoma na kuwatibu.  

Suala la Maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi, Mhe. Naibu waziri alisemawizara imeweka mkakati wa kudhibiti maambukizi mapya ya Ukimwi na kufubza virusi vya Ukimwi kupitia mkakati wa 90, 90, 90 ambao unatekelezwa sambamba na mkakati wa kupima na kuanza tiba mara moja. Pia alielezea kuhusu kampeni inayoendelea kutekelezwa kuhusu upimaji wa virusi vya ukimwi kwa wanaume ambao kiwango chao ni kidogo sana ukilinganisha na wanawake nchini wanaojitokeza kupima.  Hivyo kampeni inatekelezwa kwa kuwafuata wanaume sehemu zote walipo kama sehemu za uvuvi, sehemu za viwanda, sehemu za kunywa pombe na kuangalia mpira na sehemu za uchimbaji madini.

Kwenye suala la UKIMWI aliendelea kuelezea kuwa wizara ipo kwenye mchakato wa kupitia upya sera, sheria na taratibu za upimaji wa virusi vya ukimwi ambapo mabadiriko hayo yatawawezesha mteja kujipima mwenyewe virusi vya ukimwi bila ridhaa au uwepo wa mtoa huduma za afya. Pai njia rahisi zaidi ya upimaji zinatarajia kuanzishwa kama upimaji wa Virusi vya Ukimwi kupitian kipimo cha Kinywa ambacho mhusika ataingiza kipimo mdomoni na kusoma matokeo ya Kipimo akiwa peke ake na kipimo hiki itasaidian sana kuondoa unyanyapaa.

Aidha, alijumuisha kwa kusema kuwa upatikanaji wahuduma bora za afya katika Halmashauri ni kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi wa vituo vya kutolea huduma ambavyo kwa sasa vinapokea Fedha za Malipo kwa Ufanisi (RBF) hvyo Fedha hizi zinatakiwa zionshe matokeo ya uwepo wake kwa kutoa huduma bora za Afya. Alihitimisha kwa kusema kuwa alitamani uwepo wa Wakurugenzi, waganga wakuu wa Halmashauri zote za Mkoa, na wabunge wote wa Mkoa ili waje washuhudie Kupongezwa kwa Halmahsuri ya Nyanghwale iliyoongoza kwenye utoaji wa Huduma bora za Afya.

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Eng. Robert Gabriel alimuahidi mheshimiwa Naibu waziri kuwa Mkoa wa Geita suala ya Huduma bora zaAfya ni Kipaumbale chake hivyo ziara yake imeamsha juhudi za kuenddelea kusimamia na kufuatilia utoaji wa Huduma bora zaAfya mkoani Geita. Na ndipo alipoagiza kuwa Watoa Huduma wote kwenye vituo vya kutolea Huduma vyote Mkoa wa Geita wahakikishe kuwa amama Mjamzito na watoto wachanga wawe vipaumbele vya kwanza katika kuwahudumia pia uwepo mpangilio mzuri wa kuhakikisha vipimo vyote wanavyostahili wavipate.

Aidha kuhusu Ugonjwa wa Ukoma alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa aandae mpango kazi wa kampeni kubwa ya kutokomeza Ugonywa wa ukoma katika Mkoa wa Geita na awasilishe mpango huo ofisini kwake ndani ya wiki moja. Kuhusu suala la Mwitikio mdogo wa upimaji kwa wanaume aligiza Mganga Mkuu wa Mkoa aandae ratiba ya kutembelea maeneo yote ya makubwa ya wanaume ili wawezse kupimwa Virusi vya Ukimwi.

Aidha kwa Halmashauri ambazo hazikufikia zaidi yta asilimia 80 ya vituo vya kutolea huduma kupata nyota tatu za Tathmini ya Matokeo Makubwa sasa (BRN) kuhakikisha kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa anapata Taarifa kutoka kwa Waganga wakuu wa Wilaya hizo kuelezea ni kwanini hawakufikia kiwango cha Wizara ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.   

Baada ya kupokea Ngao ya Ushindi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale Ndugu Carlos Gwamagobe alimuahidi Mhe naibu waziri kuwa wilaya yake itaendelea kutoa huduma bora zaidi za Afya ili wakati mwinginge tushinde kwa asilimia 100.” Kama inawezekana kushinda tuzo hii tena basi sisi tutaipata mara kwa mara”… alisema Mkurugenzi.

Aidha, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Dokta Emmanuel Kadelya alimuahidi Naibu waziri kuwa ataendelea kujituma zaidi na timu yake ili kuhakikisha anapata Ngao hiyo kwa mafra nyingine tena kwa zaidi ya asilimia 93 za upimwaji za sasa.

Hafla hii ilihudhuriwa na waheshimiwa wabunge mbalimbali wa Mkoa wa Geita ambapo walionesha shauku ya kwenda kujituma zaidi kwenye Wilaya zao hatimae wakati mwingine nao waweze kupata tuzo kama Nyanghwale. “Naishika Ngao hii ya Tuzo sio kama siumii, naumia  tena nawapongeza sana Nyanghwale kwa kushinda ila kama kwenye mchezo kuna kushinda na kushindwa basi nawahakikishia kuwa tuzo hii mwakani itakua ya wilaya yangu”… alisema Mhe. Joseph Kasheku  (Musukuma) Mbunge wa Geita.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved