• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Zahanati kila Kijiji kumkomboa Mwanawake Wilayani Nyang’hwale

Posted on: March 9th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Mhe, Hamimu Gwiyama amewasihi Wananchi wa Wilaya hiyo kujitoa kwa hali na Mali kuchangia Ujenzi wa Zahanati kwenye vijiji vyao kwani Serikali itawaunga Mkono kuhakikisha  Vijiji vyote vinapata Zahanati ili Wanawake na Jamii kwa Ujumla wapate Huduma ya Afya kwenye maeneo yao.

 Aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia Wananchi wa kijiji cha Mwasabuka kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Hussein Nassor, ambapo aliwapongeza Wananchi wa Kijiji hicho kwa kuanzisha Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao.

“Tukipata Zahanati kila kijiji itasaidia kusogeza Huduma ya Afya kwa Jamii na hasa Wanawake ambao ndio wanateseka Zaidi kufuata huduma hii umbali mrefu” alisema.


Kwa Ukali,  alikemea Jamii kuacha kuwapa Mimba Wanafunzi kwani limekua tatizo kubwa sana Wilayani hapa kwani  Wanafunzi Hamsini na Mbili (52) wa Msingi  na Sekondari walipata Ujauzito na kukatiza masomo yao ndani ya mwaka 2017 pekee. Kwenye suala hilo aliwataka wanaume kuacha mara moja tabia ya kuwaoza mabinti zao mapema kwa tamaa ya kupata ng’ombe kama Mahari kwani tabia hiyo inawanyima haki ya Msingi ya kupata Elimu.

Akijibu Risala iliyosomwa na Mwalimu Neema Samweli kwa niaba ya Wanawake Wilayani, Mhe. Gwiyama aliwataka Wanawake kujiunga kwenye Vikundi na kuvisajili Kisheria ili waweze kupata Mkopo kutoka kwenye Taasisi za Fedha. “Undeni Vikundi na Mvisajili Kisheria na muwekeze hata kwa kununua Ardhi itawasaidia sana Kukopesheka na Kuboresha Miradi yenu” alisisitiza.


Awali Mhe. Gwiyama aliwahakikishia Wanawake wa Wilaya ya Nyanghwale kuwa watapata maji safi na Salama kwani Serikali inaendelea na Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria ambao utagharimu zaidi ya Bilioni 22 hadi kukamilika.

Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Rajab Mmunda alielezea juhudi za Halmahsuri katika kumkomboa Mwanamke ambapo alisema Ofisi yake inawajali na Kuwathamini sana Wanawake na kwenye kuwainua kiuchumi tayari ndani ya miezi Mitatu Halmshauri imeshatoa Shilingi Milioni Thelathini kwa vikundi mbalimbali vya Wanawake.

Kwenye Elimu alisema Uandikishwaji wa Watoto wa Kike Shule za Msingi mwaka huu umeongezeka kwa 71% ukilinganisha na mwaka jana. Alifafanua pia kuwa Ufaulu wa Watoto wa Kike kwa Shule za Msingi  umepanda kwa 85% na 49% kwa Sekondari.

Maadhimisho hayo yalienda sambamba na zoezi la Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho ambapo Mgeni Rasmi alishiriki kwenye Ujenzi huo na baadae aliendesha Harambee ambapo Wananchi na Viongozi walichangia Fedha taslimu, Mifuko ya Saruji na Nondo.

Kauli Mbiu ya Kitaifa kwa ya Siku ya Wanawake Duniani 2018 ni “ Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini”.



Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved