• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WANANCHI WAKABIDHIWA MIRADI MIWILI YA TASAF

Posted on: May 25th, 2023

Wananchi wa Kata za Shabaka na Nyijundu zilizopo Halmashauri ya Wilaya Nyang’hwale,wamekabidhiwa miradi miwili ya maendeleo iliyotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF. Miradi hiyo iliyokamilika imekabidhiwa jana Mei 24, 2023 na Katibu Tawala Wilaya, akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji Wilaya, pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.


Miradi hiyo miwili ni bweni la wanafunzi wasichana wa Shule ya Sekondari Nyijundu iliyopo kata ya Nyijundu, lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi themanini (80) na nyumba moja yenye Uniti (Apartment) mbili iliyopo Shule ya msingi Wenzura kata ya Shabaka.

Akiwasilisha taarifa za miradi hiyo, Mratibu wa TASAF Wilaya, Bw. Dalius Nyanda, alisema kuwa mradi wa jengo la bweni umegharimu kiasi cha Tsh. 157,328,023.54. na jengo la nyumba ya walimu umegharimu kias cha Tsh. 92,410,714.29. Pia, ujenzi wa majengo yote hayo mawili umehusisha nguvu na michango ya jamii.

Aidha, Katibu Tawala Wilaya ya Nyang’hwale, Bw. Fabian Yinza aliwasihi wanafunzi na walimu kuitunza miundombinu ya majengo hayo kwa kuzingatia matumizi bora, usafi, na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti maeneo yote yanayozunguka majengo yote ya taasisi.

Sambamba na hilo aliwasisitiza viongozi wa vijiji, kata na watendaji mbalimbali wa Halmshauri, kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha, muda wa mradi kukamilika, na kufuata taratibu za manunuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Bi. Husna Toni aliwahimiza wananchi kujitolea nguvu zao na kuchangia fedha, ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa. Pia, aliwasisitiza wazazi na wanafunzi kuchangamkia fursa ya uwepo wa bweni kwa kuhakikisha wanafunzi wananufaika na uwepo wa bweni hilo.

Katibu Tawala Wilaya alimalizia kwa kutoa shukran za dhati kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilaya ya Nyang’hwale. Pia, aliwasihi wanafunzi, walimu na wazazi kushirikiana kudhibti vitendo vyote vinavyosababisha kuzorota kwa taaluma, ikiwa ni pamoja na utoro, mimba kwa wanafunzi na ndoa za utotoni.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved