• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

ZIARA YA MADIWANI YA KUBADILISHANA UZOEFU NA HALAMSHAURI ZINGINE

Posted on: February 23rd, 2024

Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. John I. John, Jana Februari 22, 2023 wamefanya ziara ya kubadilishana uzoefu katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Mkoani Shinyanga.

Ziara hiyo imejikita katika kuangazia utekelezaji wa miradi ya kimkakati, namna bora ya ukusanyaji wa mapato, uendeshaji wa kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi, namna ya kuibua fursa za uwekezaji na utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.

Msafara huo wa Waheshimiwa Madiwani ulipata fursa ya kutembelea maneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyobuniwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kahama kupitia Baraza la madiwani  la Manispaa hiyo.

Sehemu hizo ni pamoja na Jengo maalumu la wagonjwa wa nje (OPD) lilipo katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama, ambapo jengo hilo limesheheni vifaa vya kisasa vya matibabu na huduma za kibingwa.

Wakiwa kwenye jengo hilo, Waheshimiwa madiwani walipata fursa ya kuingia kwenye wodi maalumu ya matibabu ya mazoezi tiba (Physiotherapy), ambapo wamejionea vifaa tiba maalumu na vya kisasa kwa ajili ya wagonjwa wenye matatizo ya viungo.

Aidha walipata fursa ya kutembelea eneo maalumu lililotengwa  kwa ajili ya shughuli za viwanda. Eneo hilo limetoa fursa kubwa kwa vijana kujiajiri kwa kufanya shughuli za ujasiriamali wa viwanda vidogovidogo na hata vikubwa. Shughuli hizo ni pamoja na  useremala, uhunzi, ufundi wa aluminium, uchomeleaji na nyingine nyingi.

Katika Jengo la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Waheshimiwa madiwani walipata kujionea namna ambavyo kituo hiko kinafanya kazi ya kuwajengea uwezo wajasiriamali na Wananchi kwa ujumla katika kuziendea fursa kupitia taasis mbalimbali zinazotoa huduma kwenye kituo hiko kama vile SIDO, TBS, VETA, TRA, na kadhalika.

Kituo hiko kinajumuisha huduma za utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu, kuongeza thamani bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo, Ushauri wa kisheria na kibiashara, kuwajengea uwezo Wajasiriamali wadogo, wa kati na Wakubwa, na kuwaingiza kwenye soko la mnyororo wa thamani.

Waheshimiwa madiwani wamefurahishwa sana na kujifunza juu ya ubunifu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama katika kuhakikisha inatoa huduma bora kwa Wananchi wake na inafikia lengo la ukusanyaji wa mapato kwa kiwango kikubwa.

Ziara hiyo itaendelea tena leo, Februari 23, 2024 Katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita.












Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved