• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WENYEVITI WA VIJIJI WATAKIWA KUTIMIZA MAJUKUMU BILA KUJALI TOFAUTI ZA KISIASA - DC KINGALAME.

Posted on: December 18th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Mhe.Grace Kingalame jana Desemba 17, 2024 amefungua mafunzo ya Uongozi kwa Wenyeviti waliochagulia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliyofanyika Novemba 27, 2024.

Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa jengo la Utawala la Hospitali ya Wilaya ya Nyang'hwale.

Akizungumza katika mafunzo hayo na Wenyeviti wateule Mhe. Kingalame amewataka Viongozi hao kutumia mafunzo hayo vyema kwenye kutekeleza majukumu katika Vijiji vyao bila kujali tofauti za Kisiasa ili kuweza kuleta maendeleo katika Vijiji hivyo.

Aidha mafunzo hayo yalijikita katika kuwakumbusha Wenyeviti wa Vijiji majukumu yao na majukumu ya Watendaji wa Vijiji ili kujua majukumu wanayopaswa kufanya katika Vijiji Vyao, pia walipewa elimu  ya Mapato ya kijiji ikiwa ni Ruzuku, michango ya Wananchi, Wafadhili pamoja na namnai ya kukusanya Mapato na namna ya kuibua Miradi kupitia Uibuaji wa fursa na Vikwazo ulioboreshwa (O&OD).

Vilevile timu ya Wakufunzi kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma Ndg. Petro Nziku na Ndg. Boaz Mbundu wamewasisitiza Wenyeviti wa Vijiji wote kushirikiana na Watendaji wa Kata na Vijiji katika kuleta maendeleo na Ustawi wa Jamii inayowazunguka.

Pamoja na mambo mengine Afisa Uchaguzi Wilaya Ndg. Dickson Msumari ametumia fursa hiyo kuwapongeza Wenyeviti wote kwa kufanikiwa kushinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 na kuwatakia utekelezaji mwema wa  majukumu yao kama walivyoaminiwa na Wananchi.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved