• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WATUMISHI WAPEWA SEMINA KUHUSU MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

Posted on: June 7th, 2023

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale wamepewa semina kuhusu umuhimu wa maadili ya Utumishi wa uma. Hayo yameelezwa jana Juni 6, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale.

Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu  Mkoa Geita, Bw. Herman Matemu, alieleza maadili kuwa ni namna ya kufikiri kwa makini katika kufanya maamuzi kuhusu mema na mabaya. Alisema kuwa maadili ni turufu muhimu sana kwa mtumishi wa uma anayotakiwa kuishi nayo katika muda wake wote wa utumishi.

Bw. Matemu aliongeza kwa kuainisha viwango vya maadili vya kuzingatia kwa mtumishi wa uma kuwa ni pamoja na uadilifu, kuheshimu sheria, kuzingatia haki na kutopendelea, kuwa muwazi, uwajibikaji, uaminifu na ukweli, matumizi sahihi ya taarifa na kuepuka mgongano wa maslahi.

Aidha, Afisa TAKUKURU kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa Geita, Bw. Said Lipunjage alielezea kuhusu umuhimu wa mtumishi wa uma kutojihusisha na vitendo vya rushwa. Pia alieleza baadhi ya makosa ambayo Mtumishi wa uma anapaswa kuepukana nayo ili asiangukie kwenye sheria inayohusiana na makosa ya rushwa.

Bw. Lipunjage aliongeza kwa kutaja baadhi ya makosa hayo kuwa ni Hongo, kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri, rushwa ya ngono, kutumia mamlaka vibaya, kutoa maelezo ya uongo kwa Afisa wa TAKUKURU, kula njama ya kutenda au kutendeka kwa kosa na kujifanya Afisa TAKUKURU.

Bw. Matemu alimalizia kwa kuelezea umuhimu wa utunzaji na udhibiti wa taarifa na siri za ofisi. “Ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza katika jamii, mtumishi wa uma anatakiwa ahakikishe anatunza taarifa zote za siri ambazo  zina hadhi ya kuwa ni siri za ofisi” Alisisitiza.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved