• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA UANDAAJI WA MASHAMBA YA SHULE KUELEKEA MSIMU WA KILIMO

Posted on: September 16th, 2025

Katibu Tawala (W) ya Nyang'hwale, Ndg. Kaunga Amani leo Septemba 16, 2025 ameongoza kikao cha Tathimini ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha robo ya nne kuanzia Mwezi Aprili hadi Juni, 2025 kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Akiwa katika kikao hicho Katibu Tawala amewataka Watendaji wa Kata kwa kushirikiana na Walimu kusimamia uandaaji wa Mashamba ya Shule kuelekea msimu wa Kilimo ili Wanafunzi waweze kupata Chakula Shuleni.

Aidha, Amemuagiza Afisa Kilimo (W) Ndg. David Mabula, kuhakikisha unafanyika uzalishaji wa kutosha wa mbegu za viazi Lishe ili Shule zote ziweze kupata Mbegu hizo kwa uhakika na zinazojitosheleza.

(Katibu Tawala  wa Wilaya ya Nyang'hwale Ndg Kaunga akitoa Maelekezo katika kikao cha lishe kwa kipindi cha robo ya nne)

Afisa Lishe Ndg. Furaha Nicholaus amesema shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo kutoa elimu ya Lishe juu ya mtindo bora wa maisha na ulaji unaofaa kwa Watumishi 11 wa TAKUKURU.

Ameongeza kuwa, yamefanyika Maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe ya Kijiji (SALIKI) ambapo Wataalamu wametoa elimu sahihi ya kuwaandalia Watoto chakula chenye virutubishi na umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya Mama kwa Watoto yaliyofanyika katika cha Nyakaswi, Nyang'hwale na Ibambila.

(Katibu Tawala Ndg Kaunga akiwa akisikiliza maoni ya Wajumbe kwenye kikao cha lishe kwa kipindi cha robo ya nne)

Halikadhalika, kampeni ya utoaji wa Matone ya Vitamin A na dawa za minyoo ya tumbo kwa Watoto wa umri miezi 6-59 imetolewa ambapo jumla ya Watoto 45,806 wamefikiwa katika Vituo vyote vya kutolea huduma.

Pia, kitengo kimeendelea kusimamia Club za Lishe katika Shule za Sekondari ambapo Shule mbili za Sekondari ya Kanegele na Kharumwa zilitembelewa kwa ajili ya kuhamasisha uanzishwaji na uendeleaji wa huduma za Chakula Mashuleni.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 02, 2025
  • TANGAZO LA KUHAMA KWA STENDI YA MABASI YA ABIRIA KWENDA STENDI MPYA YA IKANGALA KUANZIA TAREHE 30/08/2025 August 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU August 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA MKATABA July 30, 2025
  • View All

Latest News

  • WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA UANDAAJI WA MASHAMBA YA SHULE KUELEKEA MSIMU WA KILIMO

    September 16, 2025
  • WAFUGAJI WATAKIWA KUCHANJA MIFUGO YAO DHIDI YA UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU

    September 16, 2025
  • VIJIJI 09 KUNUFAIKA NA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

    September 15, 2025
  • VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA VYATAKIWA KUTHIBITI UTOROSHAJI WA ZAO LA DENGU

    September 11, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved