• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Wasichana 2523 kupata Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi Wilayani Nyang'hwale

Posted on: April 27th, 2018

Wilaya ya Nyang’hwale inatarajia kuwafikia Watoto takribani 2523 na kuwapa Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Kizazi ikiwa ni kuhakikisha tunawakinga Watoto wa Kike dhidi ya Ugonjwa huu hatari.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Ndugu Hamimu Gwiyama ameeleza hayo siku ya Jumatano wiki hii wakati wa Uzinduzi wa Chanjo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV VACCINE) nchini kwa wasichana wenye umri wa miaka Kumi na Nne (14) na Maadhimisho ya wiki ya Chanjo.

Aidha kutokana na Mafunzo yaliyoambatana na Uzinduzi huo, aliwataka viongozi wa dini kwenda kuwaeleza ukweli wananchi juu ya umuhimu wa Chanjo hiyo ili kuwatoa hofu ya aina yoyote ya tafsiri tofauti zilizopo kwenye Jamii zetu.

Mhe, Gwiyama aliwasihi wataalamu wanaotoa Chanjo hiyo kuhakikisha wanakua waadilifu na kwenye zoezi hilo ili kutoa Chanjo yenye viwango vinavyotakiwa. “Wataalamu mnaokwenda kutoa Chanjo hii nawakumbusha kuwa kuna Viwango vya dawa kwa kila mtoto anayepatiwa Chanjo hii hivyo nawasihi nendeni mkawe waadilifu huko ili kufanikisha adhma ya Serikali.”  

Vilevile, alisisitiza kuongeza Uhamasidhaji kwa Jamii ili wananchi waelewe umuhimu wa Chanjo hiyo na kutoa Chanjo kwa asilimia mia moja (100&) tuliokusudia.

Awali wakati anatoa salamu za Ufunguzi, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Phinias Ndalo alieleza kuwa Chanjo hiyo hutolewa kwa Wasichana wenye umri wa miaka 14 ikiwa ni baada ya Utafiti kuonesha Msichana anayejihusisha na Ngono katika umri mdogo ndio anakua hatarini zaidi kuambukizwa Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Kizazi uenezwao na Virusi aina ya Human Papilloma.

Aidha, Mratibu wa Chanjo Ndugu Elias Martin alifafanua kuwa dalili za Mtu aliyeambukizwa Saratani ya Mlango wa Kizazi kuwa ni Kutokwa na Uchafu Ukeni, mabadiliko ya Hedhi na Maumivu ya Mgongo au kiuno. Aliongeza kuwa Saratani ya Mlango wa Kizazi husababishwa na Kujamiiana katika Umri mdogo, kuvuta sigara, Ndoa za Mitara, Kuzaa Watoto wengi na kuwa na wapenzi wengi.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved