• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WANANCHI TUIUNGE MKONO SERIKALI KWA KUSHIRIKI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: April 18th, 2024

Wananchi wa Kata za Shabaka na Kaboha wamesisitizwa juu ya ushiriki wao wa moja kwa moja kwenye shughuli za miradi ya maendeleo. Hayo yameelezwa jana Aprili 17, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame alipofanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za Wananchi wa Kata hizo.

Mhe. Kingalame kabla ya kufanya mkutano na Wananchi hao, alikagua baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika kata hizo ambapo ameelekeza baadhi ya changamoto alizobaini kwenye miradi hiyo  zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Baadhi ya miradi aliyoitembelea ni pamoja na Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Shabaka, ujenzi wa matundu ya vyoo 10 wenye thamani ya Tsh. Milioni 28 kutoka Serikali kuu  na  ujenzi wa matundu ya vyoo 16 wenye thamani ya Tsh. Milioni 47.1 katika Shule ya Msingi Nyamgogwa.

Aidha amekagua pia ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Lubando na Zahanati ya Kijiji cha Kaboha wenye thamani ya Tsh. Milioni 50 kwa kila Zahanati. Ukamilishaji wa Zahanati hizo utasaidia  kusogeza huduma za Afya  kwa Wananchi kwa kupunguza adha ya  kutembea umbali mrefu kufata huduma za Afya.

Akiwa kwenye Mkutano wa kusikiliza kero za Wananchi wa Kata hizo, Mhe. Kingalame amewaeleza Wananchi hao kuwa Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa dhati kusogeza huduma kwa Wananchi kwa kusikiliza na kutatua kero zao.

Hivyo, amesema ni wajibu wa Wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali yao kwa kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye shughuli za miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa  sehemu mbalimbali za Wilaya ya Nyang’hwale ikiwa ni pamoja na miradi ya Elimu na Afya.

Ziara hiyo itaendelea leo Aprili 18, 2024 katika Kata ya Nyabulanda na Kata ya Mwingiro.








Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved