• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WAGONJWA ZAIDI YA 270 WAMENUFAIKA NA UJIO WA MADAKTARI BINGWA WA MAMA SAMIA

Posted on: June 28th, 2024

Kambi ya Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wilayani Nyang’hwale imewanufaisha wagonjwa zaidi ya 270 wenye magonjwa mbalimbali kwa muda wa siku tano tangu walipowasili hapo Juni 24, 2024.

Hayo yameelezwa leo na Kiongozi wa timu ya madaktari hao ambae pia ni Daktari Bingwa wa magonjwa ya Watoto, Dkt. Mariam Gaitani. Aidha, ameambatana na Daktari Bingwa wa Wanawake,  Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani, Daktari Bingwa wa upasuaji na Daktari Bingwa wa usingizi na ganzi salama.

Dkt. Mariam amesema kuwa lengo la kampeni hii ni kuhakikisha huduma bora zinawafikia Wananchi katika maeneo yao ili kuwapunguzia gharama ya kusafiri umbali mrefu kufata huduma hizo.

“Tangu tumefika hapa Jumatatu tumefanikiwa kuwaona wagonjwa zaidi ya 270, kwa hiyo muitikio wa Wananchi ni mkubwa na Wananchi wenye kuhitaji huduma kama hizi ni wengi. Hivyo, kutokana na uwepo wetu hapa, wagonjwa wamefanikiwa kupata walichokihitaji” Dkt. Mariam

Pamoja na Wananchi kunufaika moja kwa moja na ujio wa madaktari hao, Watoa huduma pia wa Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale wamenufaika kupata ujuzi kwa vitendo kutoka kwa madaktari hao.

“Kuna watoa huduma zaidi ya thelathini ambao sisi tumeweza kuwaelekeza mambo mengi ambayo baada ya sisi kuondoka wataweza kuendelea kuwahudumia Wananchi kwa kutumia Utaalamu ambao wameupata kutoka kwetu” Amesema Dkt. Mariam

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Ndugu, Husna Toni amewashukuru sana Madaktari Bingwa kwa kutoa huduma kwa Wananchi kwa kipindi chote cha siku tano katika Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale.

Kwa kumalizia amemshukuru pia Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujio wa madaktari hao Wilayani Nyang’hwale, kwani umekua na faida kubwa kwa Wananchi na Watoa huduma wa Hospitali ya Wilaya kwa kuongeza ujuzi kwa vitendo.

Kambi ya Madaktari Bingwa ilikua ya siku tano, kuanzia Juni 24, 2024 na imemalizika leo Juni 28, 2024.





Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved