• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WAFUGAJI WATAKIWA KUCHANJA MIFUGO YAO DHIDI YA UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU

Posted on: September 16th, 2025

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang’hwale Ndg kaunga Amani, leo Septemba 16, 2025, amezindua zoezi la chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Mapafu ya Ng’ombe ijulikanayo kwa jina Contagious Bovine Pleuropneumonia (CBPP) na Uvikaji Hereni kwa ajili ya Utambuzi wa Ng’ombe katika kata ya Nyabulanda Kijiji cha Nyashilanga .

(Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang'hwale Ndg, Kaunga Amani akiwataka wafugaji kuchanja mifugo yao ili kuvutia soko la kimataifa)

Akizungumza na Wafugaji Ndg, Kaunga amewataka wafugaji kujitokeza kuchanja Mifugo yao ili kudhibiti vifo vya ghafla kwa mifugo dhidi ya ugonjwa wa mapafu ya ng’ombe sambamba na uvikaji wa hereni ambazo zitasaidia kutoa taarifa za mmiliki wa ng’ombe.

Katibu Tawala amesema Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoa jumla ya dozi 1,700 ambazo zitachanja ng’ombe 170,000 zitakazomuwezesha mfugaji kulipa gharama ya Tsh. 500 tu, badala ya Tsh. 1,000 kwa kila ng’ombe.

(Afisa Mifugo akivalisha hereni ng'ombe kwa ajili ya utambuzi wa mifugo)

“Mifugo iliyochanjwa ni salama kwa matumizi ya kitoweo na itaweza kununuliwa na wafanyabiashara kutoka nchi za nje na kumnufaisha mfungaji, huku nchi ikipata fedha za kigeni” Amesema

Aidha, amekabidhi Vishikwambi 20 Kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Maafisa Mifugo ngazi ya Kata kwa ajili ya kuhifadhi taarifa za wafugaji ikiwa ni Idadi ya Mifugo anayomiliki mfugaji na mashamba ya kulisha mifugo yake.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Ndg. Ezekiel Ntiriyo amesema wafugaji wanatakiwa kushirikiana na wataalamu wa mifugo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kikamilifu na kuondoa imani potofu juu ya zoezi zima la uchanjaji.

(Katibu Tawala Wilaya ya Nyang'hwale Ndg, Amani Kaung akiwa katika picha ya Maafisa Mifugo)

Kwa upande wake mfugaji Ndg. Hamis Shija ameishukuru Serikali kwa jitihada inazozifanya katika sekta ya Ufugaji na amewahimiza wafugaji wengine watoe ushirikiano kikamilifu kwa wataalamu ili zoezi liweze kufanikiwa.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 02, 2025
  • TANGAZO LA KUHAMA KWA STENDI YA MABASI YA ABIRIA KWENDA STENDI MPYA YA IKANGALA KUANZIA TAREHE 30/08/2025 August 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU August 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA MKATABA July 30, 2025
  • View All

Latest News

  • WATENDAJI WA KATA WATAKIWA KUSIMAMIA UANDAAJI WA MASHAMBA YA SHULE KUELEKEA MSIMU WA KILIMO

    September 16, 2025
  • WAFUGAJI WATAKIWA KUCHANJA MIFUGO YAO DHIDI YA UGONJWA WA HOMA YA MAPAFU

    September 16, 2025
  • VIJIJI 09 KUNUFAIKA NA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI

    September 15, 2025
  • VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA VYATAKIWA KUTHIBITI UTOROSHAJI WA ZAO LA DENGU

    September 11, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved