• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Wafanyakazi waonywa kujihusisha na vitendo vya Rushwa

Posted on: May 1st, 2019

Mkuu wa Moa wa Geita Mhe. Robert Gabriel amewataka Wafanyakazi Mkoani Geita kutojihusiha na vitendo vya Rushwa kwenye utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwani inapelekea upotevu wa Fedha za Serikali.

Amesema hayo kwenye Viwanja vya Shule ya Sekondari Chato alipokua akiwahutubia Wafanyakazi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yalipoadhimishwa Kimkoa.  “Ubora wa Miradi unapungua panapotokea Rushwa” alisema Mkuu wa Moa.

Aidha amewataka Wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii na maarifa na nidhamu huku wakifuata miiko ya kazi zao ili kuwaletea wananchi maendeleo. “Nidhamu, heshima na kujituma iwe kipaumbele cha kwanza kwenye Mkoa wetu” alisema Mkuu wa Mkoa.

Kutia mimba Wanafunzi na kuwatumikisha Watoto ni Miongoni mwa mambo aliyokemea na ndipo akaagiza Viongozi wote kuanzia ngazi ya Vitongoji kutofumbia macho wahalifu wa aina hiyo na wataobainika wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hizo chafu Mkoani Geita. “Haki ya Mtoto ni Elimu, nawasihi viongozi kwenye maeneo yote muhakikishe mnakomesha ajira kwa Watoto”

Mhe Robert amewaahidi Wafanyakazi kuwa Changamoto zote zinazowakabili Wafanyakazi zitatatuliwa na Serikali kwani ni sikivu na amewataka pia kutatua wenyewe zile zilizo kwenye uwezo wao kiutendaji.

Aliwasihi wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI Kuhudhuria kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya ili waweze kuoata dawa za kufubaza makali na kwa wale ambao hawajajitambua basi wafike hospitali wapime afya zao ili waweze kujitambua na kuishi vizuri.

Awali Mwenyekiti wa Vyama vya Wafanyakazi Mkoa (TUCTA) mkoa wa Geita, Ndugu Ramadhani Pangala alibainisha changamoto za Wafanyakazi Mkoani Geita kuwa ni pamoja na baadhi ya waajiri kutoa mikataba ya Muda mfupi sana wa kazi,Mfuko wa Mafao wa psssf kushindwa kutoa Mafao kwa Wafanyakazi waliokuwa PSPF, wanasiasa kuingilia shughuli za Kitaalamu na kuleta hasara Serikalini,Uhaba wa Watumishi, Wafanyakazi Kuondolewa kwenye Utumishi bila Barua, kutokuwepo kwa huduma za OSHA NA WCF, na kutopewa zawadi kwa Wafanyakazi Hodari.

Bwana Pangala risala yake ilisheheni changamoto za Wafanyakazi akizitaja zingine kuwa ni  malimbikizo ya madeni kwa Watumishi, mishahara midogo, kuchelewa kupandisha vyeo, Madaraja na mishahara, Wafanyakazi wanaopandishwa Madaraja kutolipwa kwa wakati, na baadhi ya wafanyakazi wa Migodini kulipwa mishahara kupitia Serikali za Mtaa.

Kutokana na changamoto hizo alishauri Serikali kuwahamishia Watumishi wote wanalipwa mshahara kupitia Mapato ya Ndani kuwahamishia Hazina pamoja na aliomba Serikali kulipa stahiki za likizo kupitia Hazina na sio waajiri. Aidha hakusita kuipongeza Serikali kwenye uamuzi wake wa kuendelea na kikokotoo cha awali cha Mafao na sio kipya cha psssf kinachokandamiza wastaafu.

Madhehebu ya Dini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Taasisi binafsi na za Serikali kutoka wilaya zote za mkoa wa Geita  wameshiriki Maadhimisho ya Mei Mosi 2019.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved