• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

WADAU WA ELIMU WILAYANI NYANG’HWALE WAFANYA TATHMINI YA HALI YA ELIMU

Posted on: January 9th, 2024

Kikao kazi cha kutathmini hali ya elimu wilayani Nyang’hwale kimefanyika jana Januari 08, 2024 katika Ukumbi wa Bwalo la Shule ya Sekondari Msalala. Kikao hiko kimejadili mambo kadha wa kadha yanayohusu mustakabali wa elimu Wilayani humo.

Kikao kazi hiko kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame, na kuhudhiriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya pamoja na wadau wote wa sekta Elimu.

Wadau hao ni pamoja na  Wathibiti ubora wa shule (W), Tume ya utumishi wa Walimu (W) (TSC), Wenyeviti wa bodi za Shule na kamati za shule, watendaji wa kata, maafisa elimu kata, Wakuu wa shule na Walimu wakuu na walimu wa taaluma.

Kupitia mkutano huo, maswala muhimu yamejadiliwa ikiwa ni pamoja na kudhibiti tatizo la utoro, umuhimu wa chakula shuleni, uboreshaji wa mazingira ya kufundishia na kutathmini hali ya ufaulu.

Mkuu wa Wilaya, Mhe, Grace Kingalame amesema ni muhimu wadau wote wa elimu kushirikiana kwa pamoja ili kukuza kiwango cha elimu na kupata matokeo yaliyo bora zaidi.

“Kwenye hili ndugu zangu lazima tufanye kwa pamoja, walimu mpo hapa na wazazi mpo hapa, sasa niwaambie kuwa hakuna kazi ya mmoja, Mzazi ana sehemu yake na Mwalimu ana sehemu yake, kwa hiyo lazima tufanye kwa pamoja” Alisisitiza Mhe, Kingalame

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri, Ndugu Husna Toni amesema kuwa Nchi yetu inaendelea kuleta mandeleo kila kukicha katika kila sekta, na maendeleo hayo yanaenda sambamba na maswala ya elimu.

“Nchi yetu imejipambanua vizuri kuhakikisha inaboresha miundombinu inayohusiana na elimu, kuna shule mpya zinajengwa, madarasa mapya yanajengwa. Katika kata zetu karibu kila kata kuna mradi wa kielimu unajengwa” Aliongeza Mkurugenzi

Nae Katibu msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Ndugu, Shija Ngassa ameeleza kuwa mwenendo na tabia za walimu wa Wilaya ya Nyang’hwale ni nzuri kwa ujumla. Kwa mwaka 2023 Mashauri machache sana yamewasilishwa na mwajiri kwenye ofisi ya TSC kuhusu kadhia ya walimu kukengeuka na maadili ya taaluma.

Kikao hiko ni sehemu ya mikakati ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale kwa mwaka 2024 katika kuhakikisha inajiweka vyema na kusimika misingi thabiti ya kuboresha  sekta ya elimu kwa kuwashirikisha wadau wote wa sekta hiyo.

 







Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved