• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

VIJANA WATAKIWA KUWATUNZA NA KUWATHAMINI WAZEE

Posted on: October 2nd, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Jana Oktoba 1, 2024 imeadhimisha Siku ya Wazee duniani kwa kujumuika kwenye hafla ya pamoja na Wazee kutoka sehemu mbalimbali katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Msalala.

Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Diwani wa Kata ya Kharumwa, Mhe. Leonard Mgema, amesema kuwa ni muhimu kuwathamini na kuwaenzi Wazee kwa kuwa ni hazina ya hekima, maarifa, na utamaduni wa Taifa.

Wazee wakiandamana kuelekea Ukumbi wa Mikutano wa shule ya sekondari Msalala.

Mhe. Mgema ametoa wito kwa jamii kuendelea kuwatunza wazee kwa kuwapa haki zao, kuwahudumia na kuwahakikishia usalama wao katika kipindi chote cha maisha yao.

Aidha Mhe.Mgema ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Wazee kupata huduma bora za afya na kupewa kipaumbele pindi wanapokuwa kwenye maeneo ya kutolea huduma hizo ili kuwaondolea adha mbalimbali zinazoweza kujitokeza.

Mratibu wa Maadhimisho ya wazee Ndg Zaituni Kiboga  akiwasilisha ujumbe kwa Wazee

Halikadhalika, Mhe. Mgema amewakumbusha Wazee wajibu wao wa kuwalea vijana katika misingi ya Maadili na uadilifu kwa kuwakemea pale wanapokengeuka ili kuwa na jamii yenye na vijana wenye heshima na busara.

Maadhimisho hayo yametoa fursa kwa Wazee kushiriki shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na maandamo, michezo na burudani za nyimbo,na mashindano ya michezo ya jadi.

Wanafunzi wakifanya maigizo katika kusherehesha Maadhimisho hayo

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wazee Wilaya ya Nyang'hwale Mzee Eliasi Chasama amemshukuru Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya kwa kuona umuhimu wa kujumuika na  Wazee hao katika Siku hiyo muhimu.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Wazee mwaka 2024 yamesindikizwa na kauli mbiu isemayo “Tuimarishe Huduma kwa Wazee, Wazeeke kwa Heshima”

Mwakilishi wa mkuu wa Wilaya na Diwani wa kata ya Kharumwa Mhe. Mgema akitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya maigizo

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved