• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

TUUHIFADHI MSITU WA MIENZE KWA MAENDELEO ENDELEVU

Posted on: October 24th, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame, akiwa na Kamati ya Usalama (W), Kamati ya Siasa (W), na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W) kwa pamoja wamefanya ziara ya siku 3 kutoa Elimu juu ya umuhimu wa kutunza hifadhi ya msitu wa Mienze.

Hifadhi ya Msitu wa Mienze ni miongoni mwa hifadhi za misitu kongwe iliyoanzishwa mwaka 1956 kwa GN namba 104, ukiwa na ukubwa wa hekta 8988, na kwa sasa linasimamiwa na Sheria ya Misitu namba 14, ya mwaka 2002.

Kutokana na ongezeko la wingi wa watu kadri miaka inavyosonga mbele,kumekua na uhitaji mkubwa wa ardhi kwa jamii zinazoizunguka  hifadhi ya msitu huo, ambapo imezalisha uvamizi wa kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya msitu huo.

Kwa kuliona hilo, Serikali iliunda timu ya mawaziri nane wa kisekta kutathmini uhalisia wa uhitaji wa ardhi kwa wananchi walio karibu na hifadhi ya msitu huo. Serikali kupitia kamati hiyo iliridhia kutoa hekari 1852 kwa kijiji cha Bujura Mienze na hekari 331 kwa Kijiji cha Ihushi, na maombi ya vijiji vingine yakiendelea kuchakatwa.

Kwa kutambua umuhimu wa uhifadhi ya Msitu huo  Viongozi wa Serikali na Chama kwa pamoja wametembelea vijiji vya Wavu, Shabaka, Bujura Mienze, na Nyakaswi kwa lengo la kuunganisha nguvu za pamoja katika kutoa elimu na uelewa mpana kwa jamii juu ya umuhimu  wa uhifadhi wa msitu huo.

Mhe. Kingalame amesema kuwa Wananchi wanapaswa kuheshimu mipaka ya hifadhi ya msitu kwa kuwa mipaka hiyo imewekwa kisheria. Pia, amewasihi wajitokeze kwa wingi kuomba sehemu ya ardhi ambayo imekwisharidhiwa na serikali kutumika kwa shughuli za kiuchumi na makazi.

Aidha, Afisa Maliasili na uhifadhi  wa Mazingira (W), Ndugu, Mrema Juma, amesema kuwa Msitu una faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata hali ya hewa nzuri, kupata mvua kwa misimu miwili kwa mwaka, kuwezesha shughuli za ufugaji wa nyuki na biashara ya hewa ya Ukaa.

Katibu Mwenezi CCM (W), Ndugu, Said Madoshi, amewatahadharisha wananchi hao, kutofanya shughuli za kilimo wala ufugaji katika hifadhi ya msitu huo, kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria. Amesisitiza pia waliovamia maeneo hayo watoke haraka bila ya kusubiri nguvu itumike kuwaondoa.

“Kabla hawajachukua hatua hawa watu wa ulinzi na usalama , tunataka tuwaeleze , msikie, na muelewe Watanzania wa Bujura Mienze. Tumekuja kuwaeleza ukweli kwamba tokeni msituni kwa kauli ya serikali, achieni maeneo hayo, ukikutwa huko msituni, ni wewe na serikali” Alisisitiza Ndugu Madoshi.

Kwa upande wake, Afisa Ardhi (W), Ndugu, Goodluck Massatu, amewasisitiza Wananchi hao kuongeza kasi ya kuchangamkia fursa ya kuomba kumilikishwa ardhi ambayo tayari Mhe. Rais ameridhia igawiwe kwa Wanachi hao.

“Serikali imetoa hekari 1852 kwa ajili ya matumizi ya Wananchi wa Kijiji cha Bujura Mienze. Wakati Serikali inatoa eneo lile, ilitoa na maelekezo ya kufanya mpango bora wa matumizi ya ardhi na kutoa hati miliki za kimila kwa kila Mwanakijiji wa Bujura Mienze” Amesema Ndugu Masatu

“Tulikubaliana kwenye mkutano wa hadhara maeneo haya, akiwepo Mwenyekiti wa Kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, Diwani wa kata hii na Wananchi, kwamba kila atakayeomba hekari moja ya ardhi atalazimika kulipa shilingi 40,000/= kwenye akaunti ya Serikali ya Kijiji ili tuwape hati miliki ya kimila ambayo kisheria haina ukomo” Amesisitiza Ndugu Masatu



Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved