• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

THAMANI YA FEDHA IONEKANE KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI

Posted on: January 23rd, 2024

Hayo yameelezwa jana Januari 23, 2024 kufuatia ziara ya Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Nyang’hwale ambayo imekagua miradi ya maendeleo  iliyopo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyang’hwale, Ndugu, Adam Mtole.


Ziara hiyo pia imejumuisha viongozi mbalimbali wa Wilaya ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. John I. John, na Kaimu Mkurugenzi, Ndugu Majagi Maiga.


Aidha, miradi ambayo imetembelewa na kukaguliwa ni Ujenzi na ukamilishaji wa Zahanati ya Ng’wabuyi iliyopo Kijiji cha Mwingiro, Ukamilishaji wa vyumba vinane vya madarasa vya Shule mpya ya Sekondari Itetemia, na Ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Nyang’hwale.


Pia Kamati hiyo ilifika kukagua ukamilishaji wa Zahanati ya Kijiji cha Bugombela iliyopo Kata ya Nyamtukuza, Ukamilishaji wa Jengo la Utawala la Halmashauri na Kutembelea Kikundi cha akina mama “TUJIKOMBOE" kilichopo kata ya Kharumwa.


Akiwa kwenye ukaguzi wa miradi hiyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ndugu Adam Mtole amesema kuwa ni muhimu thamani ya fedha iweze kuonekana kwenye miradi yote inayotekelezwa Wilayani Nyang’hwale.


“Nimeelekeza utekelezaji wa miradi hii uendane na thamani ya fedha iliyokusudiwa na miradi ikamilike kwa wakati ili tuweze kurahisisha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi wetu”. Amesema Ndugu, Mtole


Katika hatua nyingine amesema kuwa si vyema wakati wa utekelezaji miradi hii kujihusisha na vitendo vyovyote vya ubadhilifu kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume na maadili na vinadumaza kasi ya maendeleo.


Wakiwa kwenye mradi wa ukamilishaji wa jengo la Utawala la Halmashauri  Wajumbe wa kamati hiyo ya siasa wameridhishwa na kasi kubwa ya maendeleo ya ujenzi huo kwa kuwa hali ya hivi sasa inaridhisha  ukilinganisha na hapo awali.


Ziara hiyo itaendelea leo, Januari 24, 2024 kwa kuendelea kutembelea na kukagua miradi mingine inayoendelea kutekelezwa Wilayani Nyang’hwale.













Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved