• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

SERIKALI YAIMARISHA KANUNI ZA WAJIBU WA WAMILIKI WA LESENI ZA MADINI KWA JAMII (CSR)

Posted on: October 20th, 2023

Katika kuhakikisha Jamii inayozungukwa na shughuli za uchimbaji wa madini inanufaika na shughuli hizo, Serikali imeboresha Utaratibu wa Wamiliki wa leseni za madini juu ya namna ya kuwajibika kwa Jamii kwa kuunda kanuni zinazotoa mwongozo wa utekelezaji wake.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 19, 2023, kupitia kikao maalum kilichoandaliwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Bulyanhulu inayofanya shughuli zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Msalala iliyopo Mkoani Shinyanga.

Kikao hiko maalumu kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame, akiwa na  Kamati ya Usalama (W), Wataalamu kutoka Tume ya Madini, Mkurugenzi Mtendaji (W), Ndugu, Husna Toni na Wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi.

Hapo awali, Kampuni zinazomiliki leseni za uchimbaji wa madini hazikua zikiongozwa kikanuni za namna ya uwajibikaji wao kwa jamii iliyo karibu na shughuli za uchimbaji. Hivyo basi, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeona tija ya kuunda kanuni hizo kwa maslahi mapana ya jamii na serikali kwa ujumla.

Mtaalamu kutoka Tume ya Madini, Ndugu Kasmili Daudi, wakati akitoa mada kuhusu kanuni hizo alieleza kuwa, mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kuandaa mpango madhubuti wa wajibu wake kwa jamii kwa kushirikisha Halmashauri ya Kijiji au Mtaa uliopo katika eneo lenye shughuli za  madini kupitia Halmashauri husika.

Aidha, Jamii zilizopo au zinazozunguka eneo lenye shughuli za madini zitanufaika na mpango wa wajibu kwa jamii (CSR) kwa utaratibu wa kiasi cha asilimia 40 kitatengwa kwa ajili ya miradi ya kijiji au mtaa ambapo shughuli za madini zinafanyika, na kiasi cha asilimia 60 kwa ajili ya miradi mingine ya Halmashauri. Alieleza Ndugu, Kasmili

Kanuni hizo zinaelekeza kuwa, Kila Halmashuri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji ambako shughuli za madini zinafanyika itaundwa “Kamati ya Wataalam  kuhusu Wajibu wa Mmiliki wa Leseni ya Madini kwa Jamii”.

Kamati hiyo itaundwa na Mkurugenzi Mtendaji (Mwenyekiti), Afisa Mipango (Katibu), Afisa wa Tume ya Madini wa eneo husika, wawakilishi wawili wa mmiliki wa leseni ya madini, Mhandisi, Wakili wa Serikali, Afisa Mazingira, Aafisa Maendeleo na Afisa kutoka katika mradi mahsusi unaotekelezwa.

 Hivyo,Mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kutekeleza mpango wa wajibu wake kwa jamii kwa kuzingatia taratibu za ununuzi na Halmashauri itawajibika kusimamia utekelezaji wa mpango  ikiwa ni pamoja na kukagua mikataba yote, makadirio ya kiasi (BOQ) na nyaraka zinazohusiana utekelezaji wa mpango



Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved