• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Sakata la Mimba kwa Wanafunzi Nyang’hwale, Waitara atoa Maagizo Mazito

Posted on: November 30th, 2018

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara ameagiza kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria Mwalimu Juma Magori wa shule ya Msingi Bukungu kwa tuhuma za Kumpa Mimba Mwanafunzi wa Shule hiyo.

Alibainisha hayo hayo leo alipokua akizungumza na Viongozi na Watumishi mbalimbali kwenye kikao cha Kujadili tatizo la Mimba Wilayani Nyang’hwale kama alivyoagizwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipobaini hilo mapema wiki hii alipokua kwenye ziara ya kikazi Wilayani humo.

Akizungumza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo Mhe. Waitara amesema Serikali haitavumilifu uhujumu wa aina yoyote kama watia mimba kwani hao ni sawa na wahujumu wa Miradi kwani sekta ya  Elimu Mhe. Rais amewekeza sana.

Ameagiza pia kukamatwa kwa mwananchi Rafael Mathias anayetuhumiwa kumtorosha Mwanafunzi Flra Cosmas wa Kidato cha tatu shule ya sekondari ya Njijundu.

Aidha, Mwalimu athuman Andrew Kisabo aliyetuhumiwa kwa kujihusisha na mapenzi na Mwanafunzi Magreth Zakayo naye atakamatwa na kuchukuliwa Hatua za kisheria.

Kuhusu suala la utoro ambapo imebainika kuwa kata ya Busolwa inaongoza kwa kuwa na Watoto watoro themanini na tano, Mhe. Naibu Waziri ameagiza kukamatwa kwa Watoto hao na kuwafungulia mafaili ya maelezo mara moja.

Vilevile, Mtoto Semeni Pima aliyekuwa mwanfunzi wa darasa la sita shule ya Msingi Lyulu na kuolewa, Mhe. Naibu waziri ameagiza akamatwe mtoto huyo na Kuhojiwa hadi amtaje aliyemuoa ili achukuliwe Hatua za kisheria.

Ameagiza kutafutwa na kumamatwa kwa Kijana Bundala Nyanda aliyemuoa Mwanafunzi wa darasa la tatu ajulikanaye kwa jina la Sara huko Lyulu.

Vile vile Mhe. Naibu waziri ameagiza kutafutwa kokote aliko Mwalimu Shabani aliyekuwa Mkuu washule ya sekondari ya Msalala anayetuhumiwa kwa kumuoa Mwanafunzi na alipobainika alihamishwa shule na kushushwa cheo. Aidha kwenye hili ameagiza pia aliyetoa adhabu hiyo naye achunguzwe.

Ameagiza kuchunguzwa kwa idara za Elimu Msingi na Sekondari Wilayani hapa kwani Watumishi waliopo wana umri mwingi sehemu moja ya kazi na kusababisha kuwaharibu wakuu Watumishi Wageni kwenye idara hizo.

Pia,Mhe. Naibu Waziri ameagiza kuangaliwa upya nafasi za Walimu wakuu, Watendaji wa Vijiji, Watendaji wa Kata, Waratibu wa Elimu wa Kata zote zenye tatizo kubwa la mimba kwa Wanafunzi na apewe taarifa ya hatua zitakazochukuliwa kwa watumishi hao.

Vilevile ameagiza kuhojiwa kwa Mheshimiwa wa Viti maalumu wa kutoka Busolwa Mhe. Katoto kuhojiwa kwa kushiriki kuficha wahalifu wa Mimba kwani amekua akiwadhamini wahalifu hao pilisi.

Agizo kwa Mhe. mkuu wa Wilaya amemtaka ndani ya Siku thelathini kutoa maelezo ya namna gani atatua tatizo la Mimba kwa Wanafunzi kwenye wilaya yake.

Mhe. Waitara amewaasa Viongozi wanafumbia macho Masuala ya Mimba kwa Wanafunzi na Utoro kuacha mara moja tabia hiyo kwani wasipofichua wahalifu nao wanageuka kuwa wahalifu na adhabu yao iko jikoni.

Jeshi la Polisi wilaya amelitaka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kwani sasa wananchi wameshapoteza imani na Jeshi hilo Wilayani hapa kwa tuhuma za Rushwa.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Hamimu Gwiyama aliahidi kutekeleza Maagizo yote atayopewa na Mhe Naibu Waziri na alisema vita ya Mimba ni ya watu wote hivyo viongozi hawapaswi kutupiana lawana bali kushirikiana kutokomeza Mimba kwa Wanafunzi Wilayani humo.

Akitambulisha Wajumbe wa Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauir Bi. Mariam CHaurembo alitaja sababu za Mimba kwa Wanafunzi Mashuleni kuwa ni pamoja na Tamaa kwa Wanafunzi wenyewe, Mila na desturi za Jamii ya Kuwalaza Watoto wa kike kwenye vijumba vya nje mbali na wazazi, kesi za Mimba kutofikishwa Mahakamani, Watoto kuishi mbali na shuleni na Maisha ya Gheto kwa Wanafunzi.

Jumla ya Wanafunzi Mia moja na sitini na moja (161) wametiwa mimba na kupoteza masomo yao kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi sasa Wilayani Nyang’hwale, taarifa iliyopatikana baada ya Mhe. Naibu waziri kupokea taarifa za mimba kutoka kwa watendaji wa kila kata mapema leo kwenye kikao.

 Kikao hicho kilihudhuriwa na Watumishi wasimamizi wa Serikali za Mitaa kutoka Mkoani, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Maafisa Tarafa, Watendaji wa Kata, Waratibu wa Elimu wa Kata, Walimu wakuu wa shule za Sekondari na Msingi na Wenyeviti wa Vijiji

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved