• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

PONGEZI KWA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2022, NYANG’HWALE.

Posted on: May 23rd, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale kupitia mradi wake wa kuinua ufaulu kwa shule za sekondari, ujulikanao kama Performance Imrovement Project (P.I.P), leo Mei 23, 2023 imezipongeza shule zilizofanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne 2022. Pongezi hizo zimetolewa kwa kuwagawia zawadi mbalimbali kwa wanafunzi, walimu, wazazi na shule kwa ujumla, kulingana na matokeo waliyopata kwenye mtihani huo uliofanyika mwaka jana, 2022.

Akitoa historia fupi ya mradi huo, Afisa Taaluma Elimu Sekondari Wilaya ya Nyang’hwale, Bw. Christopher Makoye alisema kuwa, mradi huo ulianzishwa mwaka 2019 ukiwa na lengo la kila shule ya sekondari iliyopo ndani ya mipaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, inahakikisha wanafunzi wanaofanya mtihani wa kidato cha nne wanakua na ufaulu wa daraja la kwanza kuanzia idadi ya wanafunzi kumi (10) na kuendelea.

Aidha alieleza kuwa, tekelezaji wa mradi huo hufanyika kwa kuhakikisha kunakua na upatikanaji wa chakula cha wanafunzi wa kidato cha nne na walimu, ununuzi wa vitabu vya rejea na kiada, na utoaji wa motisha kwa walimu, wazazi na shule zilizofanya vizuri.

Bw. Christopher Makoye alisema, tathmini inaonesha kuwa mradi huo wa kuinua ufaulu kwa shule za sekondari unaleta matokeo chanya kwa kuwa kumekua na ongezeko la ufaulu wa daraja la kwanza na ubora wa matokeo yote kwa ujumla.

Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Fabian Yinza  Akishirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya, Mhe. Husna Toni. waligawa zawadi ya fedha taslimu na zawadi nyengine mbalimbali kwa wanafunzi, walimu, wazazi na shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mtihani huo.

Sambamba na hilo, Katibu Tawala alisisitiza kuwa, Walimu, Wazazi, Watendaji wa kata na Wenyeviti wa vijiji washirikiane katika kuzishughulikia changamoto zote zinazosababisha kuzorota kwa ubora elimu. Alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na utoro, mimba kwa wanafunzi, na ndoa za utotoni.

Katibu Tawala alimalizia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hasssan na wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kuendelea na juhudi za kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved