• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Pikipiki za Waratibu wa Elimu kuboresha Elimu Nyang’hwale

Posted on: October 19th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mhe. Hamimu Gwiyama amewataka Waratibu wa Elimu ngazi wa Kata kwenda kuzitumia Pikipiki walizopewa kuboresha ufuatiliaji ili kuinua Kiwango cha Ufaulu kwa shule za Msingi na Sekondari.

Amesema hayo jana alhamis kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wakati akikabidhi Pikipiki kumi na tano kwa Waratibu wa Elimu wa kata zote kumi na tano za Wilayani hapa zilizotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia kupitia Mradi wa LANES, pamoja na Vifaa Vya Tiba vilivyotolewa na Wafadhili wa USAID BORESHA AFYA.

Mhe. Gwiyama amewataka wasimamizi hao wa Elimu kwa ngazi ya Kata kuhakikisha wanazitumia Pikipiki hizo kuzifikia shule zao na sio kukaa Ofisini na kuacha elumu ikishuka. “Kwenye Elimu bado hatujafanya vizuri, sekondari mwaka jana tulipata divisioni one sita tu, sasa vitendea kazi mmepata nasi tunataka matokeobora”.alisema Mkuu wa Wilaya.

Aidha, Mhe Gwiyama amewataka idara ya Afya kuhakikisha wanatoa Mafunzo kwa wataalamu watakaokwenda kuvitumia vifaa hivyo kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuvitunza vifaa hivyo visiharibike kwa kuvitumia visivyo.

Mbunge wa Jimbo la Nyangh’hwale Ndugu, Hussein Nassor alimshukuru Serikali kwa kutoa Vitendea kazi hivyo na kuwataka watendaji hao kwenda kuvitumia vifaa hivyo kama ilivyokusudiwa.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyangh’hwale alimshukuru Mheshimiwa Rais na Serikali ya awamu ya tano kwa msaada huo na akaahidi kuvitumia vifaa hivyo kama ilivyopangwa kwa manufaa ya Halmashauri anayoisimamia.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi wa wilaya ya Nyang’hwale Ndugu, Gervas Bidogo aliwasihi waratabu wa Elimu kutokwenda kuzitumia Pikipiki hizo kama boda boda kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamekiuka matakwa ya Vitendea kazi hivyo kwenye kuboresha Elimu.

Awali, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nyangh’hwale ndugu Emmanuel Kadelya alitambulisha vifaa vilivyotolewa na Wafadhili hao kuwa ni pamoja na ‘Vacuum Extractor’ kifaa cha kinachomsaidia mama kujifungua mtoto anapokaribia kutoka na mama akaishiwa nguvu. HBB Resuscitor, kifaa cha kumsaidia mtoto kupumua endapo atazaliwa akiwa na shida ya kupumua.

Ultra Sound, ni Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na wafadhili hao ambapo vifaa hivi hutumika kutambua jinsia ya mtoto pamoja na ulalo wa Mtoto na atapooneka kuwa amelala vibaya basi itamsaidia daktari kufanya upasuaji kwa mama huyo ili kuokoa uhai wa mama na mtoto. Infant Weighing Scale pia ni Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ambapo hutumika kupima uzito wa mtoto mara tu anapozaliwa na endapo atakua na uzito mdogo sana atawekwa kwenye chumba maalumu kwa uangalizi.

Meza, viti, Bembea za Watoto, mipira wa kuchezea mpira wa miguu na pete, Runinga na Vifaa vya Music ni Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa na Wafadhili hao kwa ajili ya kuboresha Huduma za Afya kwa vituo vya Afya Kharumwa na Nyang’hwale Wilayani hapa.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved