• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

NYANG’HWALE YAPIGA KASI HATUA ZA MAENDELEO

Posted on: December 4th, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ni miongoni mwa Halmashauri zinazokua kwa kasi katika sekta mbalimbali za maendeleo. Hayo yamaeelezwa katika kikao maalumu cha Kamati ya Maendeleo ya Wilaya kilichoketi jana  Disemba 04, 2023 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale.

Kikao hiko cha kamati kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame, kimejadili mambo kadha wa kadha ya maendeleo katika sekta za Elimu, Afya, Biashara,Kilimo, Ardhi, utawala na Maendeleo ya Jamii.

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji (W), Afisa Mipango (W), Ndugu, Utali Makwea, amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ilikasimia kukusanya Tsh. 3,070,835,930.00 na kufanikiwa kukusanya  Tsh. 3,297,959,513.06 ambayo ni sawa na mafanikio ya asilimia 107.40 zaidi ya lengo.

Katika Sekta ya Elimu, Idara ya Elimu Sekondari, Halmashauri ilitekeleza ukamilishaji wa vyumba vya maabara, hosteli katika shule mbili, nyumba za walimu, matundu ya vyoo na kutekeleza mpango wa kuinua ufaulu (PIP) ambao ulitekelezwa kwa fedha za CSR.

Aidha, katika Idara ya Elimu Msingi, Halmashauri pia ilitekeleza mradi wa Ujenzi wa Shule mpya, “Shule ya Msingi Busengwa” yenye jumla ya madarasa 16, matundu ya vyoo 24 na jengo la utawala 1, ambapo ujenzi huo megharimu jumla ya Tsh. Milioni 540.3 fedha kutoka serikali kuu kupitia mradi wa BOOST.

Kupitia mradi huo wa BOOST Halmashauri pia imetekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa mapya 23 na matundu ya vyoo 18 katika shule nyingine tano za msingi. Ambapo ujenzi huo pia uligharimu jumla ya Tsh. Milioni 620.5 na miundo mbinu hiyo imeshaanza kutumika.

Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale, Mhe. Hussein Nassor, akichangia katika kikao hiko, amesema kuwa Wananchi ni sehemu ya miradi inayoendelea kutekelezwa, hivyo ni muhimu kuhakikisha wanashirikishwa kwa kiasi kikubwa.

“Ili kuweka mazingira mazuri ya Wananchi kushiriki na kuweza kuchangia kwenye miradi ya maendeleo ni muhimu Watendaji wa Kata muwe mnawasomea Wananchi mapato na matumizi” Amesema Mhe. Nassor

Mkuu wa Wilaya, Mhe. Grace Kingalame, ametoa wito wa kudhibitiwa kwa tatizo la utoro kwa Wanafunzi, ambapo ameelekeza Watendaji wa Kata kuwachukulia hatua stahiki bila kumwonea mtu kwa wazazi wote watakaobainika kuwa watoto wao hawahudhurii shuleni.

Akiendelea kuwasilisha taarifa hiyo, Ndugu Utali alisema kwenye sekta ya Afya, hatua mbalimbali za maendeleo zimefikiwa ikiwa ni pamoja na ukamilishaji wa Zahanati, ukamilishaji wa wodi ya kisasa na jengo la dharura katika Hospitali ya Wilaya, ukamilishaji wa nyumba ya mtumishi na kuwezesha kufanyika shughuli za Lishe bora.

Kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri imechangia kiasi cha Tsh. 217,228,109 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu kwa fedha za mapato ya ndani. Ambapo jumla ya vikundi 88 vimepata mikopo hiyo ya 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mazuri yote haya ni sehemu ya utashi na jitihada za makusudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kutenga fedha za kutosha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa Wananchi.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved