• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Nyang'hwale kutumia Biliomi 24 Mwaka wa Fedha 2019/20

Posted on: February 21st, 2019

Jana jumatano Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imepitisha bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 yenye jumla ya Tshs: 24,617,556,201.00 zitazotumika katika shughuli mbalimbali kwa mchanganuo ufuatao:

Makisio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020


Mishahara (Ruzuku ya Serikali)

16,444,584,000.00

Matumizi Mengineyo (Ruzuku ya Serikali)

873,106,588.00

Matumizi Mengineyo (Mapato ya Halmashauri)

449,314,000.00

Miradi: Fedha za Mapato ya Halmashauri (Own Source)

332,876,000.00

Miradi: Fedha za Ndani (Ruzuku)

2,395,909,400.00

Miradi: Fedha za Nje (Wahisani)

2,066,227,953.00

(CHF, Papo kwa Papo & NHIF)

50,000,000.00

Nguvu za Wananchi

350,000,000.00

Jumla ya fedha za ruzuku ya matumizi ya kawaida, miradi ya maendeleo na Nguvu za Wananchi, mwaka 2019/2020.

24,617,556,201.00


Akiwasilisha bajeti hiyo Afisa Mipango wa Halmashauri Ndugu Magoti Pius amesema bajeti hiyo imeshuka kwenye makusanyo ya Ndani kutoka BIlioni 1.2 ya mwaka wa Fedha unaoendelea hadi Milioni 832 kwa mwaka wa Fedha ujao kutokana na chanzo cha zao la pamba kushuka uzalishaji kutokana na mvua. Aidha ametaja pia chanzo cha Ushuru wa Huduma kutoka Mgodi wa Acacia kimeshuka kwa asilimia tisini tofauti na awali kutokana na Kampuni hiyo ya Uchimbaji wa Dhahabu kupunguza uzalishaji kwa asilimia tisini na kuathiri kodi ya Huduma wanayotoa kwenye Halmashauri hiyo.

Akiongea wakati wa kufunga Baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mheshimiwa John Isack aliwataka wakuu wa idara kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kila idara inakusanya vizuri Mapato yaliyopo kwenye idara zao. “Bajeti ya mwaka ujao tumeshaipitisha, sasa nawaagiza wakuu wa idara kukaza buti kukusanya Mapato kwa ajili ya bajeti tunayoendelea nayo na tuwe na mikakati mizuri ya kutekeleza Bajeti ijayo”….alisema.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Mheshimiwa Hamimu Gwiyama alifafanua kuhusu matumizi sahihi ya Vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo vilivyotolewa nchi nzima ambapo alisisitiza matumizi sahihi yazingatiwe kwani atakayekiuka atachukuliwa hatua za sheria ya kodi.

Aidha, Mheshimiwa Ndozi Mayala diwani wa kata ya Nyugwa aliwataka timu ya Mapato ya Halmashauri kushirikiana na Watendaji wa kata na Vijiji kwenye kufuatilia Mapato ya Makarasha na Viwanda vya kuchenjua Dahahabu kwani wao ndio wanazifahamu vizuri kazi hizo na wahusika wapo nao kwenye maeneo yao wakati wote hivyo itasaidia kupata Mapato bila kukwepa.

Baraza la madiwani wilayani Nyang’hwale limeketi siku mbili kupitia mapitio ya Bajeti ya mwaka wa Fedha unaoendelea ambayo yalionekana kukusanya kwa asilimia 28 tu  badala ya asilimia 50 mpaka sasa ikiwa ni nusu mwaka na siku ya pili limepitisha bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved