• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI WA HALMASHAURI YA WILAYA NYANG’HWALE ATOA MAELEKEZO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Posted on: September 26th, 2024

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale Ndg. Husna Toni leo Septemba 26, 2024 ametoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Maelekezo hayo ameyatoa katika Ukumbi wa Halmashauri na kuhudhuriwa na makundi mbalimbali ya Wadau wa Uchaguzi ikiwa ni pamoja na Viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa dini, Viongozi wa Wafanya biashara, Watendaji wa Vijiji,  Watendaji wa Kata na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale, Ndg. Husna Toni akitoa Maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Amesema kuwa maelekezo hayo yanafafanua hatua muhimu zitakazoongoza mchakato wa Uchaguzi kuanzia uandikishaji wa wapiga kura, uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea, uteuzi wa wagombea na tarehe ya siku ya uchaguzi.

“Maelekezo haya yanalenga kutoa mwongozo ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa wazi, haki na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa” Amefafanua

Aidha, ameeleza sifa za Mpiga Kura kuwa ni pamoja na Awe na umri wa miaka 18 au zaidi, Awe raia wa Tanzania, Awe mkazi wa eneo la Kitongoji, Awe na akili timamu na Awe amejiandikisha katika Kitongoji husika.

Sambamba na hayo ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kushiriki katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura litakalofanyika kwa siku kumi kuanzia Oktoba 11 hadi 20, 2024.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Nyang'hwale, Ndg. Kaunga Omari akitoa neno mara baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kutoa maelekezo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Pia amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi utakaofanyika siku ya Jumatano Novemba 27, 2024 ili waweze kuchagua viongozi ngazi ya Vijiji na Vitongoji.

Pamoja na mambo mengine, Msimamizi wa Uchaguzi ameeleza tarehe za kuanza na kumalizika kwa Kampeni za Uchaguzi, ambapo zitaanza Novemba 20 hadi 26, 2024 kuanzia Saa 2 kamili Asubuhi hadi Saa 12 kamili jioni.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 unaongozwa na kauli mbiu isemayo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”

Afisa Uchaguzi Wilaya ya Nyang'hwale, Ndg. Dickson Msumari akizungumza na wajumbe

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 02, 2025
  • TANGAZO LA KUHAMA KWA STENDI YA MABASI YA ABIRIA KWENDA STENDI MPYA YA IKANGALA KUANZIA TAREHE 30/08/2025 August 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU August 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA MKATABA July 30, 2025
  • View All

Latest News

  • MILIONI 206 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 31 VYA VIJANA,WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU AWAMU YA KWANZA YA MWAKA 2025/2026

    October 24, 2025
  • MKURUGENZI MKUU TAKUKURU AZINDUA JENGO LA OFISI ZA TAKUKURU NYANG'HWALE

    October 22, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WAHIMIZWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI

    October 18, 2025
  • WATENDAJI WA KATA WAJENGEWA UWEZO WA KUSIMAMIA MIRADI KWENYE KATA ZAO

    October 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved