• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI SIKU YA PILI

Posted on: February 16th, 2022

Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Isaack John kama ilivyoada alianza kwa kusoma Sara ya Halmashauri na baada ya kusoma sara alifungua mkutano wa baraza la madiwani siku ya pili mnamo saa 04:10 asubuhi. Mkutano ulianza kwa waheshimiwa madiwani kuwasilisha taarifa za utendaji kwa kamati za kudumu za Halmashauri. Baada ya kuwasilisha taarifa hizo ilifuata kipindi cha maswali na majibu ambayo yalijibiwa kwa mujibu taratibu lakini hoja kubwa ilikuwa ni swali toka kwa diwani wa mwingiro ambaye alitaka kujua wananchi wa kijiji cha ng’wasabuka wamezuiliwa kuchimba dhabahu na mgodi wa acacia nini hatima ya ushuru kwa halmashauri, majibu yaliyotolewa yakisisitizwa na Mhe. DC ni kuwa wananchi wa kijiji hicho walichozuiliwa ni shughuli ya kuchimba dhahabu lakini shughuli zingine za kiuchumi kama ufugaji na kilimo bado wanaendelea kama kawaida, dhumuni la kuwazuia ilikuwa ni kulinda usalama wa leseni ya mgodi wa acacia ambaye pia ni mdau mkubwa wa Maendeleo katka halmashauri yetu.

Kuhusu Pori la hifadhi la Miyenze kuvamiwa na wananchi ambapo mhe diwani kata ya nyugwa alieleza kuwa uhifadhi wa pori hilo ubadilishwe ikiwezekana watafutwe wanyama wakali kama simba wawekwe kwenye pori hilo ili watu wasiweze ingia kama ilivyo sasa. Mhe DC pia alieleza “Mhe Mwenyekiti baraza lako linajua Zaidi kilichotokea zoezi lililofanywa na serikali na kuamua kusitisha, kuna tume ya mawaziri nane ilikuja na kutoa maelekezo hivyo tukiwa tunasubili taratibu ni vyema sharia za kulinda misitu zifuatwe. Hoja iliyotolewa na diwani ni kuwa bado kuna wananchi wanaendelea na uvamizi wa eneo hilo, aidha baraza lako liendee kujadili aidha msitu ubaki wa asili au uwe wa kupanda pande zote mbili ziangaliwe kwa faida na hasara”.

Pia hoja ya barabara iliulizwa na mhe Mwenyekiti kumwagiza Manager TARURA atoe taarifa ya fedha zilizopokelewa zitatekeleza barabara zipi kisha aziwasilishwe kwa kila diwani ili ajue katika eneo lake.

Baada ya mjadala kuisha Mhe Mwenyekiti alimkaribisha mkuu wa wilaya atoe salama kwa wananchi waliokuwa wamehudhuria katika baraza hilo. Mhe Mkuu wa Wilaya alianza kwa kusema “ Nampongeza sana Mkurugenzi Mtendaji kwa kuendelea kuzisimamia vyema halmashauri kwa kushirikiana na wakuu wa idara na vitengo, pia kamati ya ulinzi na usalama wanafanya kazi nzuri sana si shughuli za ulinzi na usalama tu bali hata shughuli za kusimamia miradi ya Maendeleo Halmashauri, shughuli ya ukusanyaji mapato inaendelea vizuri na tukitia nia ya dhati tunaweza ongoza kitaifa”. Aliendelea kueleza kuwa kuanzia sasa kuna zoezi la anwani za makazi hivyo waheshimiwa madiwani washirikiane na watendaji kuelimisha jamii itoe ushirikiano katika zoezi ili  likamilike kwa wakati uliowekwa.

Baada ya salamu hizo mhe Mwenyekiti alifunga mkutano mnamo saa 9:10 alasiri.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved