• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

MICHEZO IIMARISHE MSHIKAMANO NA UMOJA WETU

Posted on: January 20th, 2024

Jamii nyingi zimekuwa zikitumia michezo kama nyenzo muhimu katika kuimarisha Umoja na Mshikamano wa jamii hizo. Hayo yameelezwa jana, Januari 19, 2024 katika Bonanza la michezo mbalimbali ya kuukaribisha Mwaka mpya lililofanyika Uwanja wa Sabasaba.

Bonanza hilo lilijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo, Mpira wa miguu, mpira wa pete, karata, drafti na mchezo wa bao. Ambapo sehemu kubwa ya wananchi walijitokeza kujumuika katika katika michezo hiyo.

Mchezo wa mpira wa miguu ilichezwa mechi kati ya wapenzi wa timu ya Simba dhidi ya wapenzi wa timu ya Yanga, ambapo timu ya wapenzi wa Yanga iliitandika timu ya wapenzi wa Simba kwa bao moja kwa sufuri.

Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete, ilichezwa mechi kati ya timu ya Shule ya Msingi Bupamba dhidi ya timu ya Wajasiliamali. Ambapo timu ya wajasiliamali iliichabanga magoli 28 dhidi ya magoli 20 ya timu ya Shule ya Msingi Bupamba.

Mchezo wa Mwisho ulikua unajumuisha Michezo ya jadi, ambapo mchezo wa bao mshindi alikua Ndugu, Said Kanyele, mchezo wa karata mshindi alikua Ndugu, Adam Nassor, na Mchezo wa drafti mshindi aliibuka Ndugu, Mange Fungameza.

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame akiongea na Wananchi  waliojitokeza kwenye bonanza hilo, amesema kuwa tutumie michezo kuwa ni sehemu ya kudumisha umoja na mshikamano wetu ulioasisiwa tangu hapo awali.

Mhe. Kingalame aliongeza kuwa Michezo ni Afya na Ajira pia, hivyo Wananchi wajitahidi kutumia fursa hiyo kuimarisha afya zao kwa kufanya mazoezi mara kwa mara lakini pia kubaini vipaji walivyonavyo watoto na kuhakikisha wanaviendeleza vipaji hivyo.

Aidha, alitumia Fursa hiyo pia kuwakumbusha Wazazi kuwapeleka watoto shule kwa kuwa hiki ni kipindi cha uandikishaji wa Wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kuwapokea kidato cha kwanza waliopangiwa kusoma  shule mbalimbali za Sekondari.

Imekua ni desturi kwa Wilaya ya Nyang’hwale kuukaribisha Mwaka mpya kwa aina yake, kwa kuandaa mabonanza ya michezo na hafla fupi yanayotoa fursa ya kujenga mahusiano mazuri kwa Watumishi wa Wilaya hiyo na Jamii inayowahudumia.











Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • KWA KIPINDI CHA ROBO YA TATU HALMASHAURI IMEPOKEA FEDHA TSH. BILIONI 1.1 ZA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • SIKU YA FAMILIA WAZAZI WATAKIWA KUIMARISHA FAMILIA

    May 15, 2025
  • BARRICK NA HALMASHAURI WASAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI YA CSR 2025

    May 13, 2025
  • DAS AWATAKA WAZAZI KULINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI

    May 10, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved