• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Mhe, John Isack Mwenyekiti Mpya Baraza la Madiwani Nyang’hwale

Posted on: September 23rd, 2018

Baraza la Madiwani la Dharula limeketi jana Jumamosi kwenye Ukumbi wa Halmashauri Nyang’hwale na kumchagua Diwani wa Kata ya Kafita Mhe, Isack kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri baada ya wiki iliyopita Mwenyekiti aliyehudumu miaka mitatu kujiuzulu kutokana na usimamizi mbovu wa Fedha za Miradi ya Halmashauri na kupelekea upotevu wa Fedha zaidi ya Bilioni mbili.

Kura za Ndio za Wajumbe ishirini (20) kati ya Wajumbe ishirini na moja (21) waliopiga kura zilitosha kumpa Mhe, Isack Uongozi wa juu wa Halmashauri wakati Makamu Mwenyekiti Mhe, Mashaka Jeki Diwani wa kata ya Izunya akijizolea kura zote Ishirini na Moja (21) za Wajumbe waliopiga kura.

Baada ya Uchaguzi huo ziliundwa kamati za kudumu za Halmashauri na kukamilisha safu ya Uongozi kwa kuwapata pia Wenyeviti wa kila kamati. Kamati zilizoundwa ni pamoja na Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ambayo itaongozwa na Mwenyekiti wake Mhe, Isack John Isack.

Mhe, Mageni Mageni akichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Elimu, Afya na Maji. Uchumi, Ujenzi na Mazingira ni kamati ingine ya kudumu ya Halmashauri ambapo mhe, Revocatus Jacob ameibuka kuwa Mwenyekiti.

Vile vile Mhe, Jeki Mashaka Jeki amekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Kuthibiti Ukimwi. Kamati ya Maadili sasa itaongozwa na Mwenyekiti wake Mhe, Aloyce Lubambi.

Baada ya Uchaguzi huo, Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Ndugu Hamimu Gwiyama aliwataka Waheshimiwa Madiwani kuvunja makundi yote na kuwa kitu kimoja ili kushirikiana kuijenga wilaya yao. “Kundi letu sasa ni moja tu linaitwa Maendeleo Nyanghwale” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.

Mhe, Gwiyama aliwaomba viongozi hao wapya kusimamia Halmashauri kwa uwezo wao wote ili yasitokee matatizo kama ya hapo awali. “…fomu mlichukua wenyewe, na waheshimiwa Madiwani wamethibitisha..sasa msipoteze uaminifu kwa waliowachagua” alisema Gwiyama.

Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale Mhe, Hussein Nassor aliwataka waheshimiwa Madiwani kushirikiana na viongozi wapya waliochaguliwa kuijenga Nyanh’hwale na aliwataka kufunika yaliyopita na sasa waanze upya ukurasa wa maendeleo.

Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Ndugu Sania Mwangakala aliwapongeza Madiwani kwa hatua hilo ambapo aliwataka wasianguke tena kwani kuteleza sio kuanguka na sasa wasonge mbele kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria na miongozo ya Fedha zote Halmashauri itazozipokea. Aidha Ndugu Mwangakala aliikumbusha Halmashauri kuhakikisha vikao vya kisheria kuanzia kwenye vijiji vinakaa kila wakati kwani hali hiyo itasaidia sana kubaini matatizo ya wanan chi kuanzia chini na kutatua kwa wakati.

Mhe, Adam Mtore Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Nyang’hwale alitumia nafasi hiyo kulaani tukio la upotevu wa Fedha na alisisitiza kuwa safu mpya iliyoindwa isikosee na aliwakumbusha kuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana watafanikiwa zaidi kuliko kuamua jambo mtu mmoja mmoja.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Mariam Chaurembo aliwahakikishia viongozi wote kuwa watendaji sasa wameshaelewa nini anataka kwenye utendaji wake na ameahidi kuwa yeye na timu yake sasa ni kazi tu.

Vile vile aliwaomba waheshimiwa Madiwani kushirikiana kwa pamoja na Menejimenti ya Halmashauri kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kuwafichua wanakwepa kwani wao wapo vijijini wakati mwingine wanakua na taarifa nzuri zinaweza kusaidia. “Waheshimiwa Madiwani niwakumbushe kuwa asilimia sitini ya mapato huwa yanarudi kwenu kwa shughuli za maendeleo Vijijini, asilimia kumi zinakwenda kwa wanawake na Vijana na ni asilimia thelathini tu ndio zinatumika kwa shughuli za Halmashauri” alisema Mkurugenzi.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved