• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

KIKAO CHA UZINDUZI WA MIRADI YA WASH – 2022/2023

Posted on: April 25th, 2023

Kikoa cha Uzinduzi wa Miradi ya WASH kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 kimefanyika leo tarehe 25/04/2023 kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale. Kikao hicho kilichoongozwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Wilya ambae ni Katiba Tawala Wilaya Ndugu Fabian Yinza kimekua na lengo la hakikisha Mradi yote iliyopata pesa mwaka huu inakamilika kwa Asilimia 100%

Halmashauri ya Wilaya Nyang’hwale ni miongoni mwa halmashauri 5 zinazotekeleza mradi wa Maji na usafi wa mazingira kupitia kampeni ya huduma endelevu ya maji na usafi wa mazingira vijijini. Mradi huu ulianza kutekelezwa kwa awamu ya kwanza mwaka 2019/2020, awamu ya pili 2020/2021 na kwa sasa ni utekelezaji wa awamu ya 3, 2022/2023. Kupitia mradi huu tayari matundu 46 ya vyoo yameishajengwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya 9, vifaa vya kunawia mikono vya kudumu 89 vimewekwa, vituo 7 vimenunua/kujenga matanki ya kuhifadhia maji pamoja na kuvuna maji ya mvua.

Mratibu wa WASH George Ndukwa, akiongea kwenye kikao hicho alieleza kuwa hali ya usafi ilivyo kwa ngazi wa Wilaya ni kama ifuatavyo. Vyoo bora kwa ngazi ya Wilaya ni asilimia 62%, 2021/2022 ukilinganisha na mwaka 2020/2021 hali ya vyoo bora ilikuwa ni asilimia 57.7%. Upatikanaji wa maji kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni asilimi 52% ,2021/2022 ukiringanisha na mwaka 2020/2021 ilikuwa ni asilimia 24.7%. Uwepo wa vyoo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ni asilimia 72%, 2021/2022 ukilinganisha na mwaka 2020/2021 ilikuwa asilimia 48%

Kwa upande wa Utekelezaji wa Miradi kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 Mratibu alisema, Jumla ya vituo vinane vilipangiwa kutekeleza miundo mbinu alivitaja Vituo hivyo ni, Shabaka, Mwingiro, Nyarubele, Lyulu, Kafita, Kayenze, Mwamakiliga na Nyangalamila ambapo ilikua Kujenga miundombinu ya maji tangi la chini, tangi la juu Pamoja na  kusambaza maji ndani ya jengo, Kujenga vyoo na Kujenga kichomea taka  aina de Montfort

Katika utekelezaji wa awamu ya 3 Mratibu alieleza kuwa Halmashauri imepokea kiasi cha Tsh 226,873,068/- kwa ajili ya mwendelezo wa kuboresha miundo mbinu ya maji pamoja na vyoo kwenye vituo 4 vya kutolea huduma za afya vya Zahanati ya  Nyamtukuza        29,398,802, Zahanati ya Nyamikonze  52,422,003, Zahanati ya Mhama  52,632,003, Zahanati  ya Ifugandi 58,326,300.

Aidha Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya, Ndugu Fabian Yinza aliwataka wale wote waliopewa dhamana ya Kusimamia Miradi hiyo Kuhakikisha wanafanya Kazi vizuri kwa wakati na kuzingatia ubora wa Miradi hiyo. Aliendelea Kusisitiza umakini wakati wa Utekelezaji wa Miradi hiyo kwa Upande wa upotevu wa Vifaa vya Miradi ambavyo husababisha hasara kwa Serikali. Sambamba na hilo alizungumzia maswala ya Ununuzi wa vifaa vya Miradi kuzingatia ubora na gharama ili kuwezesha miradi kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi Husna Toni kwa upande wake aliwaomba viongozi wa Vijiji na Vitongoji kuendelea kutoa elimu ya ujenzi wa Vioo kwenye jamii zao ili kuboresha hali ya Maisha. Pia alisisitiza swala la Mikataba ya Ujenzi kuzingatia Muda uliopangwa kukamilisha Miradi hiyo kwa kuhakikisha Mafundi wote watakaopta kazi za Ujenzi kwenye Miradi ya Mwaka huu kuwepo eneo laMradi muda wote wa Mkataba.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved