• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YARIDHISHWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: May 3rd, 2024

Wajumbe wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango jana Mei 02, 2024 imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambae pia ni Diwani wa kata ya Kafita, Mhe. John I. John amesema kuwa sehemu kubwa ya miradi hiyo inatekelezwa kwa kasi inayoridhisha licha ya changamoto chache zinazojitokeza.

Aidha ameongeza kuwa ni muhimu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati ili ianze kutumika kwa kutoa huduma zilizokusudiwa kwa Wananchi.

“Tumeletewa fedha nyingi na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi hii, hivyo sisi kama kamati tuna jukumu la kusimamia na kuhakikisha fedha hizo zinatumika vizuri na thamani yake ionekane kupitia miradi hii” Amesisitiza Mhe. John

Miongoni mwa miradi ambayo ilipata fursa ya kutembelewa ni pamoja na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika kituo cha Afya Nyang’hwale wenye thamani ya Tsh. Milioni 160.7, ambapo kukamilika kwake kutapunguza umbali wa kufata huduma za Afya kwa wakazi wa maeneo hayo.

Wajumbe wa kamati hiyo pia walitembelea mradi wa Ukamilishaji wa kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi wenye thamani Tsh. Milioni 247.1 ambapo ujenzi ujenzi wake umefikia asilimia 85.

Kituo hiko kitakapokamilika kinatarajiwa kuwa na faida za moja kwa moja Wananchi ambapo faida hizo zitatokana na uwepo wa Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi zitakazorahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa jamii.

Miradi mingine ni ujenzi wa  matundu saba ya vyoo, Ofisi, na kichomea taka katika stendi ya Ikangala wenye thamani ya Tsh. Milioni 62.3, Ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wenye thamani ya Tsh. Milioni 150 na mradi wa kikundi cha vijana cha uchakataji wa nafaka uliopo Kijiji cha Nyakaswi.

Ziara hiyo itaendelea leo Mei 03, 2024









Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved