• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Posted on: October 29th, 2023

Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika hatua mbalimbali Wilayani Nyang’hwale. Ziara hiyo imefanyika kwa siku mbili kuanzia Oktoba 27 hadi Oktoba 28, 2023.

Miongoni mwa miradi ambayo ilipata fursa ya kutembelewa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya ya sekondari Kanegele wenye thamani ya Tsh.  Milioni 584.2 fedha kutoka serikali kuu.  Ambapo kwa sasa mradi huo upo hatua ya upigaji wa lipu na upauaji kwa baadhi ya majengo

Ujenzi wa mradi huu unatarajiwa kuwa faida kadhaa ambazo ni pamoja na kuondoa changamoto ya Wanafunzi kutembea umbali mrefu wa kwenda na kurudi shule. Pamoja na hilo, itaondoa changamoto kwa wanafunzi  wa kike ambao wanakua hatarini zaidi wapokua njiani kuifata Elimu.

Aidha, Afisa Maendeleo ya Jamii (w), Majagi Maiga, ameishukuru serikali kwa maamuzi ya kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo. Sambamba na hilo ametoa rai kwa wazazi na Wananchi kwa ujumla kutumia fursa ya uwepo wa shule hiyo kwa kuwapeleka watoto shule ili waweze kuzifikia ndoto zao.

Wajumbe wa kamati hiyo pia walitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika Zahanati ya Kafita, iliyopo Kata ya Kafita,  ambapo ujenzi huo mpaka kukamilika kwake utagharimu jumla ya Tsh. Milioni 25, fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.

Pia, Katika Kata hiyo ya Kafita, wajumbe walitembelea kikundi cha vijana kinachofanya shughuli za usafirishaji wa abiria kwa pikipiki, maarufu kwa jina la bodaboda. Kikundi hiko chenye Wanachama watano kilipata mkopo wa fedha taslimu Milioni 5 kutoka kwenye 4% inayotengwa na Halmashauri katika mapato yake ya ndani.

“Tumefanikiwa kununua pikipiki mbili kupitia fedha tuliyokopeshwa na Halmashauri, na tumefanikiwa kutoa ajira kwa vijana wengine wawili ambao tumeingia nao mkataba.  Pia, mpaka sasa tumefanikiwa kurejesha kiasi cha Tsh. 3,600,000/= na tunaendelea kurejesha kwa mujibu wa sheria” Amesema Katibu wa Kikundi hiko

Mradi wa mwisho kutembelewa ulikua Mradi wa kukuza Uchumi wa Kaya za walengwa wa TASAF, wenye thamani ya Tsh. Milioni 22.2. Mradi huo una jumla ya mifugo 508, ambapo Mbuzi 151, kondoo 112 na kuku 245, ambao wamenunuliwa kwa ajili ya walengwa 88 kati ya 93 ambapo kufikia Novemba 1, 2023 zoezi litakua limekamilika kwa walengwa wote.

“Mhe. Mwenyekiti wa Kamati, Kupitia mradi huu walengwa wa TASAF wameimarika kiuchumi na kwa sasa wana uwezo wa kukabiliana na changamoto ndogondogo za dharura. Tunakushukuru sana wewe na Kamati yako kwa kupitisha fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu”. Amesema Mtendaji wa Kijiji cha Bukungu




Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved