• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Huduma za Uzazi Zahanati ya Nyijundu zaboreshwa

Posted on: May 19th, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale Ndugu Carlos Gwamagobe  jana mchana amekabidhi kitanda cha Kujifungulia, cha kupumzikia wagonjwa na Mashuka 12 kwenye Zahanati ya Nyijundu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Mbili.

Akikabidhi Vitanda hivyo Ndugu Mkurugenzi  amewasihi akina mama Kuhudhuria Clinic mara tu wapatapo ujauzito ili wapate Vipimo juu ya Ujauzito wao ambapo watapewa Ushauri wa Wataalamu kuhusu maendeleo ya Ujauzito.

Aidha amewasihi Wanaume kujenga Tabia ya kuwasindikiza wake zao Clinic kwani nao watapata Vipimo na Ushauri wa Jinsi ya Kuishi kwa kuzingatia Misingi ya Afya bora ambapo itawasaidia Kujikinga na Magonjwa ya Kuambukizwa na pia watapata Elimu ya Moja kwa Moja ya jinsi gani wawasaidie wake zao wakiwa kwenye hiyo hali.

Kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji cha Nyijundu Diwani wa kata hiyo Ndugu Mayunga Godfrey amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji kwa Kuwajali wanawake na wananchi wa Nyijundu kwa Ujumla na Kumwomba aendelee kutatua kero mbalimbali za wananchi wake ili kuboresha Maisha yao.

Kabla ya Hafla hiyo Ndugu Mkurugenzi alitembelea wodi ya Wazazi ya Zahanati hiyo ambapo alifurahi sana alipomkuta Bi Happiness Lusonja aliyekuwa na Mtoto mchanga wa siku moja aliyejifungulia kwenye Zahanati hiyo juzi, na alimpatia Zawadi kwa Uzazi wake na Mama Mama huyo alimshukuru sana na Kumtakia Utumishi mwema.

Amewashukuru Wahisani na Wadau Mbalimbali ambao wanaisaidia Halmashauri yetu katika nyanja tofauti ambapo alifafanua kuwa vifaa hivyo vimetolewa Kwa Ushirikiano kati ya Mkurugenzi Mtendaji aliyetoa Kitanda cha Kujifungulia, Kampuni ya Uchimbaji wa Madini ya Dhahabu ACACIA-Bulyanhulu waliotoa Kitanda cha Kupumzika wagonjwa na Mashuka na Godoro ambalo limetolewa na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale.




Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved