• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG’HWALE YAFANYA TATHMINI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIOFANYIKA NOVEMBA 27, 2024.

Posted on: December 13th, 2024

Kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale, Afisa Uchaguzi wa Wilaya Ndg. Dickson Msumari leo Desemba 13, 2024 amewasilisha taarifa ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 katika Kikao cha tathmini kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.

Tathmini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 Wilaya ya Nyang’hwale ilifanyika na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Halmashauri, Kata na Vijiji.

Akiwa katika kikao cha tathmini hiko Afisa Uchaguzi aliwasilisha taarifa ya uhamasishaji na elimu ya uandikishaji na kupiga Kura ambapo amesema uhamasishaji ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kufika kila Kitongoji na Kijiji kwa njia ya mikusanyiko, matangazo ya Magari na kushirikisha madhehebu ya Dini ambapo ilisaidia kuwa na muitikio mkubwa wa Wananchi kujiandikishaji na kupiga Kura.

Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale inatoa Shukrani za dhati kwa Mhe, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Halmashauri Fedha Tsh Billion 1.01 kwa ajili ya kununua Vifaa na Fedha za kuendeshea shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 hadi kukamilika.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ulifanyika Novemba 27, 2024 katika Kata 15, Vijiji 62 na Vitongoji 273 ambapo idadi ya Wapiga Kura waliojiandikisha ni 104,335 na walio piga Kura ni 72,035 sawa na asilimia 62 ya Wananchi waliojiandikisha kupiga Kura.

Akiendelea kuwasilisha taarifa hiyo Afisa Uchaguzi alitoa taarifa ya matokeo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na  jumla ya Vyama vilivyoshiriki vinne ambavyo ni CCM, CHADEMA, CUF na NCCR-MAGEUZI ambapo CCM ilifanikiwa kushinda jumla ya Vijiji 60 na Vitongoji 270, CHADEMA ikishinda  Vijiji viwili (2) na Vitongoji vitatu (3) huku CUF na NCCR-MAGEUZI havikufanikiwa kushinda Kijiji wala Kitongoji chochote.

Pamoja na mambo mengine Halmashauri inatoa shukrani kwa ushirikiano kutoka Kamati ya Usalama ya Wilaya na Mkoa katika kufanikisha zoezi la Uchaguzi. Vilevile shukrani ziende kwa Watumishi wote wa Serikali, Mgambo pamoja na Wadau wote wakiwemo Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini na Wazee Maarufu.

Halmashauri inawatakia kheri Viongozi wote katika kutekeleza majukumu ya kuwahudumia Wananchi wa Nyang’hwale.



Announcements

  • TANGAZO LA NAFASI 53 ZA KUKUSANYA MAPATO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANGH'WALE June 23, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI May 03, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • View All

Latest News

  • WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KULINDA HAKI ZA WATOTO

    June 16, 2025
  • NYANG'HWALE YAPONGEZWA KWA KUPATA HATI SAFI

    June 11, 2025
  • MILIONI 303 ZATOLEWA KWA VIKUNDI 53 VYA VIJANA, WANAWAKE NA WENYE ULEMAVU AWAMU YA PILI

    June 03, 2025
  • NYANG'HWALE YAZINDUA ZOEZI LA CHANJO DHIDI YA KICHAA CHA MBWA

    June 02, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved