• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

ELIMU YA AFYA YA MACHO YAENDELEA KUTOLEWA MASHULENI KUELEKEA SIKU YA MACHO DUNIANI

Posted on: October 8th, 2025

Kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Macho Duaniani Oktoba 9, Halmashauri ya wilaya ya Nyang'hwale kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Huduma za Lishe imetoa Elimu ya Afya ya macho kwenye taasisi za Umma, binafsi na Wananchi kwa ujumla.

Elimu hiyo imetolewa Jana Oktoba 7, 2025, katika Shule ya Msingi Kayenze, Shule ya Msingi Kitongo, Shule ya Sekondari Nyugwa, Benki ya CRDB, NMB na Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Elimu hiyo imetolewa na Madaktari kutoka Hospitali ya Wilaya ikiongozwa na Mratibu wa afya ya macho Wilaya Dkt, Athuman Masanja.

Akizungumza wakati wa utoaji wa Elimu ya Afya ya macho, Dkt. Athuman amesema lengo la Maadhimisho hayo ni kutoa Elimu na Huduma za uchunguzi wa macho kwa Wanafunzi na Wananchi kwa ujumla, ili kubaini mapema changamoto za uoni na kuzitafutia tiba stahiki.

Dkt, Athuman amesema katika uchunguzi wa awali wamebaini idadi kubwa ya watu wamekuwa na matatizo ya macho yanayosababishwa na Bakteria na utumiaji wa dawa pasipo maelekezo ya Daktari.

Kwa upande wake, Mfamasia  Joshua Mafuru, amewataka Wanafunzi wasitumie dawa za macho bila kupata vipimo Kutoka kwa Daktari anaehusika na macho kwa kuwa utumiaji holela wa dawa unaathiri mac

Sambamba na hayo Ndg, Mafuru  amesema tatizo la upungufu wa vitamini "A" ni miongoni mwa changamoto zinazoweza kuzuilika kwa kula vyakula vyenye virutubisho muhimu, hasa mboga za majani na matunda kama vile karoti na parachichi.

Aidha, Dkt. Eliana Timu, mmoja wa Wataalamu wa afya walioshiriki katika utoaji wa Elimu ya macho, amesisitiza umuhimu wa Wanafunzi kuwahamasisha Wazazi kuwa na desturi ya kupima Afya ya macho ambapo huduma hiyo inapatikana Hospitali ya Wilaya ya Nyang'hwale.

Maadhimisho ya mwaka 2025 yanaambatana na kauli mbiu isemayo “Penda Macho Yako, Kila Mtu Anahusika”, ambapo inaihimiza jamii kujali afya ya macho kama sehemu muhimu ya ustawi wa maisha na maendeleo.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 02, 2025
  • TANGAZO LA KUHAMA KWA STENDI YA MABASI YA ABIRIA KWENDA STENDI MPYA YA IKANGALA KUANZIA TAREHE 30/08/2025 August 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE,VIJANA NA WENYE ULEMAVU August 04, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KAZI YA MKATABA July 30, 2025
  • View All

Latest News

  • WATENDAJI WA KATA WAJENGEWA UWEZO WA KUSIMAMIA MIRADI KWENYE KATA ZAO

    October 10, 2025
  • WANANCHI WATAKIWA KUJIFUNZA ELIMU YA WATU WAZIMA KIDIGITALI ILI KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA

    October 10, 2025
  • DC KINGALAME AKABIDHI MBEGU ZA MAHINDI KWA SHULE ZOTE ZA SEKONDARI NA MSINGI

    October 09, 2025
  • MRADI WA INTER HOUSE COMPETITION WAWAVUTIA WANAFUNZI KUKAA BWENI

    October 08, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved