• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

DC Nyang’hwale atangaza Kiama kwa wanaotia Mimba wanafunzi

Posted on: December 10th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Nyanghwale Mhe. Hamim Gwiyama amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kuwakamata watu wote waliowapa Mimba Wanafunzi Wilayani Nyang’hwale na kuwafikisha kwenye vyombo vya Sheria.

Agizo hilo amelitoa mapema leo wakati akihutubia wananchi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba Wilayani Nyang’hwale.

Gwiyama amesisitiza kuwa watu wote wanaoficha wahalifu wa Ukatili kwa Watoto na Wanawake watachukuliwa hatua kwani suala la kuwalinda Watoto na akina mama dhidi ya Ukatili wa Kijinsia ni la Jamii nzima.

Amewataka Watumishi wa Umma kuzingatia maadili ya Utumishi wao na wakienda visivyo yeye atawashughulikia wote kwa mujibu wa sheria. “kuna Watumishi mnatajwa kula rushwa kwenye kesi za Ukatili wa kijinsia, hakuna atakayebaki salama”…alisema Gwiyama.

Ametumia nafasi hiyo pia kuwasihi Vijana wanaojihusisha na mahusiano na Wanafunzi kuacha mara moja kwani sasa kuna msako mkali na yeyote atakayekutwa na Mwanafunzi atakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Afande Mponjoli alikiri kuwepo kwa Vitendo vya Ukatili Mkoani humo na kusema kuwa anasikitishwa sana kwani vitendo hivyo vinakiuka Haki za Biandamu.

Afande Mponjoli aliwataka Wazazi kutekeleza wajibu wao kwenye suala la Kupinga Ukatili kwa Watoto wao kwani wao ndio walio ngazi ya chini Watoto wanakotoka.“Jamii inapashwa sasa kutambua kuwa Ukatili kwa Watoto ni tatizo, watambue pia kuwa wapo ndani ya Tatizo hilo na waone namna gani wanatoka hapo” …alisema.

Aidha, alitambulisha kuwa Uwazi, Ukweli, Weledi na Uwajibikaji kuwa ni nguzo kuu za kutokomeza Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake.

Akiwakaribisha Wageni kwenye Maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nyang’hwale Mhe. Isack John aliwataka Jamii kuwalinda wajane na Yatima waliopo kwenye Jamii zao kwa kuwapa mahitaji yao ya Msingi ili kujenga Jamii imara.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Nyang’hwale Bi. Zaituni Kiboga alieleza kuwa Idara yake inatoa Huduma za Tiba na Saikolojia kwa waathirika wa Ukatili wa Kijinsia na aliomba Jamii kutoa taarifa za Ukatili hasawa Watoto mapema ili wapatiwe huduma za Kisheria mapema.

Aidha, alitambulisha kuwa zimeundwa kamati mbalimba;I kuanzia ngazi za Vijotnoji hadi wilaya ili kupambana na vitendo vya Ukatili wa Kijinsia Wilayani humo.

Afisa Kutoka Jeshi la Polisi anayeshughulikia Masuala ya kijinsia amesema Matukio ya Ukatili wa Watoto na Wanawake Mkoani Geita yameongezeka kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo ameelezea Umasikini na imani za Kishirikina kuwa chanzo kikubwa cha matatizo hayo.

Amesema Mimba za Utotoni, Mimba kwa Wanafunzi, Ndoa za Utotoni, Kutumikisha Watoto, Unyanyapaa kwa Wajane, Kutelekeza Watoto, Kutoa Mimba, kurithi Wajane, Ukeketaji na Ulawiti ni Miongoni mwa Matukio uya Ukatili kwa Watoto na Wanawake.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved