• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang'hwale

  • Home
  • About Us
    • History
      • Origin
      • Coverage area
      • Responsible people
      • climate condition
      • Economic activities
      • List of leaders
    • Mission and Vision
    • Strategies
    • Core values
  • Adminstration
    • Organisation Structure
    • Departments
      • Administration and Human Resources
      • Solid Waste and Environmental Management
      • Finance and Trade
      • Planning, Statistics and Monitoring
      • Community Development, Gender and Youth
      • Secondary Education
      • Primary Education
      • Agriculture, Irrigation and Co-operative
      • Health
      • Water
      • Land and Natural Resources
      • Liverstock and Fisheries
      • Works
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Election
      • Internal Audit
      • Beekeeping
      • Procurement and Supplies
  • Investment Opportunities
    • Livestock keeping
    • Agriculture
    • Tourism attraction
  • Our Services
    • Water
    • Healthy
    • Education
    • Fisheries
    • Livestock
  • Madiwani
    • Councillors List
    • Standing Committee
    • Timetable
  • Projects
    • Completed projects
    • Continous Projects
    • Planned Projects
  • Publications
    • Acts
    • customer service Contract
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Different forms
    • guideliness
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

Amref wamwaga Baiskeli kwa Wahudumu wa Afya Vijijini

Posted on: May 17th, 2018

Jumatano tarehe 16, Mei 2018 Wahudumu wa afya ngazi ya Jamii Wilayani Nyang’hwale na Geita wamegawiwa baiskeli zilizotolewa na Serikali ya Canada chini ya Shirika la Amref watazozitumia kuwafikia wananchi wakati wa kuwapatia huduma.

Akiwashukuru wafadhili hao, Mhe. Hamimu Gwiyama, Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale amewataka Wahudumu kwenda kuzitumia baiskeli hizo kwa malengo yaliyopangwa ili zikasaidie kutokomeza kabisa vifo vya Watoto chini ya miaka mitano pamoja na vifo vitokanavyo na Uzazi.

Wahudumu wa Afya 124 wamenufaika na Vitendea kazi hivyo Wilayani Nyang’hwale ikiwa ni baiskeli moja kwa kila mhudumu ikiwa ni wahudumu wawili kwa kila kijiji kwa vijiji vyote 62, pamoja na baiskeli zingine 310 zilizotolewa kwa wahudumu hao Wilayani Geita.

Aidha, Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili za Nyang’hwale na Geita walielezea furaha zao kwa Serikali ya Canada chini ya shirika la Amref kwa msaada huo pamoja na mingine kama ya Ujenzi wa Vyumba vya upasuaji Viwili kwa kila Wilaya na Ukarabati wa Zahanati nne kwenye kila Wilaya, Ujenzi unaoendelea.

Awali meneja Huduma kwa Jamii kutoka Amref alifafanua kuwa wataendelea kutoa huduma kwa Wahudumu ili kuhakikisha Vifo vya Watoto chini ya miaka mitano na vitokanavyo na uzazi na tayari walishawajengea uwezo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora. Viatu na Mavazi ya kukinga ni miongoni mwa vifaa ambavyo wamewagawia siku za karibuni na watawagawia tena mabegi hivi karibuni.

Kwa niaba ya Mganga mkuu wa Wilaya, Ndugu, Alfred Chabila aliwashukuru Amref kwa msaada huo na mingi wanayotoa kwenye wilaya yetu ambapo alielezea kuwa wamesaidia sana kuongeza hudhurio la wamama wajawazito Cliniki mara tu wapatapo Ujauzito ndani ya miezi mitatu ya Mwanzo.

Aidha, alifafanua kuwa vifo vya Watoto chini ya miaka mitano kwa mwaka 2016 vilikuwa sitini na saba (67) ambapo kwa manufaa ya Huduma bora zitolewazo na Wahudumu wa Afya vijijini ilisaidia kupunguza hadi ishirini na tisa (29) kwa mwaka 2017.

Kwa pamoja wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii Wilayani Nyang’hwale walitoa kauli mbiu ya kazi yao mbele ya mgeni Rasmi isemayo ‘vifo vitokanavyo na uzazi, Watoto wachanga na watoto chini ya miaka mitano havikubaliki, tushirikiane kutokomeza’

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - KAZI YA MUDA April 27, 2025
  • TANGAZO LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI KUNDI LA WANAWAKE KIJIJI CHA SHIBUMBA KATA YA KABOHA December 06, 2024
  • TANGAZO LA KUTEULIWA KWA WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA November 21, 2024
  • TANGAZO KWA WATUMISHI. October 22, 2024
  • View All

Latest News

  • BARRICK YAFADHILI ZOEZI LA UPULIZIAJI WA VIUATILIFU KWENYE NYUMBA ZA WAKAZI

    May 08, 2025
  • WANAFUNZI WATAKIWA KUTUMIA MAJI SAFI NA SALAMA

    May 07, 2025
  • MHE. JOHN ISACK AAGIZA KIWANDA CHA NISHATI SAFI KIKAMILIKE KWA WAKATI

    May 07, 2025
  • WANANCHI WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE

    April 24, 2025
  • View All

Video

TAHADHARI JUU YA MLIPUKO WA UGONJWA WA MPOX
More Videos

Quick Links

  • Watumishi portal
  • Mwongozo wa matumizi ya TEHAMA serikalini
  • Maombi ya biashara
  • Fomu mbalimbali

Related Links

  • Tovuti ya Ikulu
  • Wakala wa serikali mtandao
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Contact Us

    Barabara ya Halmashauri

    Postal Address: 352-Nyang'hwale

    Telephone: +255 28252061

    Mobile: +255 .....

    Email: ded@nyanghwaledc.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://freehitcounters.org

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

copyright@2017 Halmashauri ya wilaya Nyanghwale.All right reserved